Ukiendelea Na Tabia Hizi Mafanikio Kwako Yatakuwa Ni Ndoto
May 12, 2017
Read
Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama
kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama
aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira
hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida
sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.
Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba
binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu
anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye
kikombe na umgorogee na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo
subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari
imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi, kitu cha
kujiuliza je, mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai
yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu.
Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema
sifanyi biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi
biashara yeyote tatizo nini? Atamsikia anakujibu tatizo mtaji huku
akiamini kuwa mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa
makala hii hata uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya
matumizi ya fedha, hata ukipewa milioni mia moja leo hizo pesa zitaisha
utajikuta mwisho wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama
mitaji kama fedha peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu
mpaka mwisho huku maisha yakiendelea kuwa magaumu.
Ngoja nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja
nguvu ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate
fedha. Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na
mawasiliano unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa
computer na kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza
vipi kubadili ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi
tunapofeli kwa sababu ni wavivu wa kufikiri.
Naendelea kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivyokuwa na
tabia za lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta anaishi mazingira machafu
ambayo yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta
binadamu huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini mazingira haya ni
machafu, utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali,
binadamu huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini hauna
ajira? Atakujibu tatizo ni serikali.
Kuna msanii mmoja wa hapa nchini aliwahi kuimba kwenye wimbo huku
akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila
kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile
ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama
unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa,
maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya
hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako
yatakuja kwa asilimia chache sana.
Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na
msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata yule unayemlalamikia
hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu
kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke
usemi huu “kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari’’
Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini
upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa kiswahili unasema kila binadamu
ni mchungaji ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga
nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi
kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma
makala hii endapo utaulizwa swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha
uone una thamani gani mbele ya watu wengine?
Ukiendelea Na Tabia Hizi Mafanikio Kwako Yatakuwa Ni Ndoto
Reviewed by Unknown
on
May 12, 2017
Rating: 5
No comments:
Post a Comment