TANESCO YAANZA KUWABANA WADAIWA SUGU WA BILI ZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM
NA Manyama Junior
“MANENO
ni mawili tu “KA na TA” ukiunganisha Kata, asiyelipa kateni umeme” Hayo
yalikuwa ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa ujenzi wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme mkoani Mtwara miezi michche
iliyopita.
Kufuatia
maagizo hayo ya Rais, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), kupitia kwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wake, Dkt. Tito Mwinuka, aliitisha mkutano
na waandihi wa habari na kutoa ilani kwa wadaiwa wote “sugu” wa bili za
umeme kuwa walipe madeni yao vinginevyo huduma ya umeme itasitishwa.
Baada
ya tangazo hilo, baadhi ya taasisi za serikali likiwemo Jesho la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance
Mabeyo, naye aliitisha mkutano na wanahabari na kueleza kuwa JWTZ
italipa sdeni lake na kuagiza wahusika wafanye hivyo mara moja.
Leo
hii Mei 4, 2017, Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius
Nangali, aliwaita waandishi wa habari ofisini kwake na kuwaeleza kuwa
taasisi za umma na binafsi zilizo katika mkoa wake, zilikuwa zikidaiwa
jumla ya shilingi Bilioni 7, ambapo taasisi za serikali pekee zilikuwa
na deni la shilingi bilioni 6 na kwa sasa tayari zimelipa jumla ya shilingi bilioni 2 na kubaki deni la shilingi bikioni 4.
“Hizi
taasisi za umma tumeingia nazo mkataba na kwakweli wameanza kulipa na
tunaendelea kuwahimiza wafanye hivyo ili wasije kukosa huduma ya umeme.”
Alisema Mhandisi Nangali.
Aidha
alisema taasisi binafsi zinadaiwa shilingi Bilioni 1 na nyingi kati ya
hizo hazijaingia mkataba wa malipo ya madeni yake na TANESCO kwa hivyo
akatahadharisha kuwa TANESCO haitasita kuchukua hatua za kusitisha
huduma ya umeme na kwa kuonyesha kuwa Shirika halifanyi mzaha, leo hii
kampuni mbili moja ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Fida Hussein
iliyoko Vingunguti wilayani humo imesitishiwa huduma ya umeme kufuatia
deni la shilingi Milioni 29.
Kampuni nyingine iliyoonja joto ya jiwe ni Iprint iliyoko
eneo la Banda la Ngozi kandokando ya barabara ya Nyerere, kampuni hiyo
hadi kufikia leo Mei 4, 2017 ilikuwa ikidaiwa jumla ya shilingi Milioni
16,95.
Maafisa
wa TANESCO waliokuwa kwenye operesheni ya “kukata” umeme kwa wadaiwa
sugu, walikuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa kufikia leo Mei 4, 2017
kampuni hizo mbili zikikuwa zikidaiwa madeni hayo.
Mafundi
wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es
Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeem, tayari kwa kazi kwenye
transfoma ya kupeleka umeem kwenye eneo la kiwanda kinachomilikiwa na
mfanyabishara maarufu jijini, Bw. Fida Hussein kilichiko Vingunguti leo
Mei 4, 2017
Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, Mhandisi Athanasius
Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao
makuu, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2017.
Mhandisi
wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza
na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint
Hii ni stakabadhi ya leo Mei 4, 2017 ikionyesha kampuni ya I print ikidaiwa shilinhi milioni 16.95
Maafisa wa TANESCO makao makuu, wakimsikiliza meneja wa kiwanda cha Fida Hussein(kulia)
Wanahabari wakiwa kazini
Mhandisi Athanasius Nangali(kulia), akiongea na waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment