Rais Magufuli Atapokea Taarifa ya Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga Saa Tatu Asubuhi Hii
Kurugenzi
 ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri
 ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo  tarehe 24 
Mei, 2017 atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza 
mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo 
katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.
Tukio
 la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na 
kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni 
na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Wananchi
 mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa 
hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment