Trending News>>

Michezo:TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA .


Image result for tetesi za usajili
1.BAYERN MUNICH imedhamiria kumsajili Fowadi wa Arsenal Alexis Sanchez ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ili iweze kuwa kali zaidi. Sababu nyingine ya Bavarians kumtaka nyota huyo ni kumuunganisha na Mchile mwenzake, Arturo Vidal. (#Sun
2.REAL MADRID inakaribia kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Flamengo, Vinicius Junior kwa dau la pauni £45m. (#Daily_Mail
3.KIPA wa Arsenal, David Ospina yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ili kujiunga nayo baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza. (#Mirror
4.ATLETICO MADRID inataka kumrudisha nyumbani Fowadi wake, Diego Costa wa Chelsea. Fowadi huyo wa Kihispania yupo kwenye mchakato wa kuelekea China kwenye klabu ya Tianjin Quanjian. (#Telegraph
5.KOCHA wa Manchester United Jose Mourinhi anataka kuwauza mabeki wake Chris Smalling na Phil Jones ili kusajili nyota wengine watakaoziba nafasi zao. (#ESPN_FC
6.BEKI wa Real Madrid Pepe yupo mbioni kujiunga na Inter Milan huku mastaa wengine kama Fabio Coentrao, Mariano, Danilo, James Rodriguez , Keylor Navas, Alvaro Morata na Gareth Bale wapo mbioni kuondoka Santiago Bernabeu msimu huu. (#Don_Balon
7.WINGA wa PSG Angel Di Maria anataka kurejea Santiago Bernabeu. Staa huyo aliondoka Real Madrid mwaka 2014 lakini anafikiria kurudi tena klabuni hapo lakini Rais wao Florentino Perez hapendi wachezaji wa Kiargentina katika kikosi chake. (#L_Equipe
8.KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane amemuweka Kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante kama chaguo lake namba moja katika nyota anaowataka Santiago Bernabeu. (#Marca
9.TOTTENHAM inakaribia kukamilisha dili la beki wa pembeni wa Fulham, Ryan Sessegnon kwa dau la pauni £12m. (#Evening_Standard
10.KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger anataka kumsajili Mshambuliaji kinda mwenye umri wa miaka 19, Henry Onyekuru raia wa Nigeria. Supestaa huyo wa Klabu ya KAS EUPEN ya Ubelgiji yupo katika kiwango cha juu msimu baada ya kufunga mabao 22 katika ligi ya Ubelgiji. (#Sky_Sports
11.KLABU ya Tianjin Quanjian ya China inataka kumsajili Fowadi wa Werder Bremen ya Ujerumani , Max Kruise. Fowadi huyo wa zamani wa Vfl Wolfsburg amefunga mabao 15 na Assist 7 msimu huu akiwa na Bremen. (#Reports
12.LEICESTER CITY & WEST BROM zipo kwenye vita kali ya kumuwania Beki kisiki wa Middlesbrough, Ben Gibson ambaye atapatikana kwa dau la pauni £20m. (#Daily_News
13.LIVERPOOL inakaribia kukamilisha usajili wa Winga wa Leicester City, Demarai Gray kwa dau la pauni £12m. Majogoo hao Anfield wanataka kumsajili nyota huyo kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa. (#Liverpool_Echo
14.BAYERN MUNICH imewaweka sokoni mastaa wake wawili, Douglas Costa na Renato Sanches. Mabingwa hao wa Ujerumani wanatafuta wabadala wa nyota wao Xabi Alonso na Philipp Lahm ambao wanastaafu soka hivyo kuamua kuwapiga bei Costa na Sanches ili kuwapata warithi wa wakongwe hao. Hata hivyo Makinda Joshua Kimmich na Kingsley Coman wamehakikishiwa kuwa watabaki Allianz Arena. (#Kicker

No comments:

Powered by Blogger.