MICHEZO:Barua ya Bodi ya Ligi kuhusu sakata la alama tatu kati ya Kagera Sugar na Simba SC.
Bodi
ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewajibu rasmi Simba SC
juu ya sakata lao la kupokwa pointi tatu za mezani walizopewa baada ya
rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar wakidai kumcheza mchezaji Mohamed Fakhi
akiwa na kadi tatu za njano.
Kwa
mujibu wa barua kutoka katika Bodi ya Ligi zimesema kuwa Fakhi hakuwa
na kadi tatu za njano wakati akicheza mchezo dhidi ya Simba uliofanyikia
uwanja wa Kaitaba, Bukoba Aprili 2 mwaka huu.
"TFF
ambayo ndiyo yenye dhamana ya usimamizi wa mpira nchini na ambayo ndiyo
iliyokaimu madaraka kwa TPLB kuendesha ligi kuu iliitisha kikao cha
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo ilichunguza kwa undani
sakata hili na baada ya uchunguzi wao ambao walihoji watu mbalimbali,
walituandikia kutujulisha kuwa wamebaini mchezaji Mohamed Fakhi
anayelalamikiwa na Simba hakuwa na kadi 3 siku ya mchezo wa Kagera
Sugara dhidi ya Simba hivyo alikuwa halali kucheza mchezo huo". Ilisema
barua hiyo
No comments:
Post a Comment