Trending News>>

Gabo Zigamba anyoosha Maelezo kuhusu Kuwa Penzini na Wema Sepetu


Gabo Zigamba amefunguka kwa kudai kuwa picha za kimahaba zilizozagaa mitandaoni akiwa na Wema Sepetu ni maandalizi ya kazi yao mpya na siyo mambo mengine.
Muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya filamu, amedai filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Heaven Sent’ ni full mahaba ndio maana picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinawaonyesha wakawa katika hali isiyo ya kawida.
“Movie tunayoifanya na Wema iko very romantic ndio maana hata picha zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi mashabiki zangu naandaa kitu kikali sana mara mbili za jinsi wanavyonifahamu,” alisema Gabo.
Pamoja na hayo Gabo amewataka mashabiki wa filamu waendelee kuwapatia changamoto za kejeli ikiwa ni pamoja na kusisistiza kazi nzuri ili wasanii wasibweteke isipokuwa kutoa lugha za matusi.

No comments:

Powered by Blogger.