Wananchi Ukerewe wapongeza Serikali kwa kasi ya miradi ya umeme
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto mbele) akibadilishana mawazo na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kwenye ziara ya kuelekea katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.
Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply kilichopo Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Sitta Ngissa (katikati) akielezea hali ya uzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya jua katika kituo hicho, Kushoto ni David Mwakigonja kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Mfumo wa kuongozea mitambo na vifaa vya kuzalisha umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kulia) akifafanua jambo kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto)
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kushoto) akieleza jambo katika chumba cha betri kwa ajili ya kuhifadhi umeme kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kulia)
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini na watendaji kutoka kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.
Mtaalam kutoka kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Mhandisi Egberth Bashuweka (kulia) akielezea kazi ya mita za umeme jua kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto).
Na Greyson Mwase, Mwanza
Wananchi wa wilaya ya Ukerewe wameipongeza serikali kwa kasi ya miradi ya umeme katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi hususan za uvuvi.
Waliyasema hayo katika nyakati tofauti jana katika ziara ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini yenye lengo la kujionea hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya miradi hiyo inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu wa Kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank Matondane alisema kuwa kitongoji hicho hakikuwa na ndoto ya kupata umeme wangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika lakini matumaini yamepatikana baada ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya umeme katika kitongoji hicho kupitia kampuni ya Rex Energy.
Alisema mara baada ya wananchi kuhamasishwa na wataalam kutoka kampuni ya Rex Energy na kuona zoezi la ujenzi wa miundombinu ya umeme, walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutodai fidia hali iliyorahisisha utekelezaji wa mradi huo.
Matondane alisema kuwa mahitaji ya umeme katika kitongoji cha Ghana/Siza chenye wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya 2,500 hadi 5,000 ni makubwa husuan wavuvi wanaohitaji umeme kwa ajili ya kwenye majokofu ya kuhifadhia samaki.
Aliongeza kuwa shule pamoja na maduka ya madawa baridi yanahitaji umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, uchumi katika kisiwa hicho utakua kwa kasi kutokana na fursa zilizopo na kuvutia wawekezaji kwenye ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama ya samaki.
Naye mmoja wa wakazi wa kitongoji hicho, Emanuel Mfungo alisema kuwa wakazi wa kitongoji hicho wameshaanza kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba zao kwa ajili ya kujiandaa na huduma ya kuunganishwa na huduma ya umeme.
Alisema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa umeme, wananchi wa kitongoji hicho weamekuwa ni walinzi wa miundombinu ya umeme ili kutohujumiwa na watu wasiotakia mema kitongoji hicho.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa akielezea hatua iliyofikiwa ya mradi huo, alisema kuwa kazi ya ujenzi wa miundombinu imeshakamilika katika kituo chote na kusisitiza kuwa kampuni inatarajia kufunga mtambo wa kuzalisha umeme kwa umeme jua wenye uwezo wa Kilowati 350 ambapo utaongezwa uwezo wake kutokana na mahitaji ya umeme katika kitongoji hicho.
No comments:
Post a Comment