Wananchi Geita Waenda mkutanoni wamebeba madumu tupu ya maji
Hali hiyo imejitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa ng’ombem lengo likiwa kusikiliza kero za wananchi na kuzipeleka bungeni ili zifanyiwe kazi na wahusika.
Wauzaji hao na wananchi waliokuwa na madumu yao yakiwa pembeni ya Mwembe, huku wakiwa wanamkisiliza mbunge huyo wamesema wanalazimika kunywa maji machafu huku dumu la maji hayo likiuzwa kwa Shs 1000, jambo ambalo ni kero kwa wananchi.
Nao viongozi wa mitaa mbalimbali ndani ya kata hiyo wamedai pamoja na kuwepo kwa miradi ya maji lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya kukwamishwa na baadhi ya watendaji.
No comments:
Post a Comment