Trending News>>

Wanafunzi zaidi ya 250 Gairo hatarini kushindwa kuanza masomo


Licha ya serikali kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini,wanafunzi zaidi ya 250 wilayani Gairo mkoani Morogoro wako hatarini kushindwa kuanza masomo kwa muhula wa kwanza 2017 kutokana na wazazi kushindwa kuwapatia watoto wao mahitaji ya shule kwa madai ya kuwepo ugumu wa maisha.
Image result for shule wilaya ya  gairo
Kufuatia tatizo hilo mkuu wa wilaya Gairo Bi.Siriel Mchemba amegawa sare za shule,viatu madaftari pamoja na kalamu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nane ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza masomo mara shule zitakapofunguliwa.

Akizungumza na wazazi mara baada ya kugawa sare hizo kwa niaba ya mkuu wa wilaya, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Gairo Agnes Mkandya amesema serikali haitawavumilia wazazi watakaoshindwa kuwapeleka wawtoto wao shule kwa kisingizio cha ugumu wa maisha hasa waliopatiwa mahitaji hayo.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliopokea msaada wa sare za shule wameshukuru mkuu huyo wa wilaya  huku wakiomba jitihada za haraka kufanyika juu ya watoto wanaositishwa masomo yao kutokana na kupata ujauzito.

No comments:

Powered by Blogger.