Waliotaka kuiba Transfoma wanusurika kifo
Watu watatu kutoka Jijini Arusha wamenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Mogitu wilayani Hanang, baada ya kukutwa wakiharibu miundo mbinu ya Tanesco na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni kumi kwa Shirika hilo la umeme.
Na hawa ni wananchi wa kijiji hiki cha mogitu wakieleza hali halisi ya tukio la kuwakamata wahusika wa kuharibu miundo mbinu ya Tanesco na hivyo kupelekea kilio hata kwananchi kukosa nishati ya umeme ambayo wamesemakuwa wanategemea katika kuendesha mitambo yao ya kuvuta maji kwaajili ya matumizi ya kila siku pamoja na kunywesha mifugo yao.
Lakini marietha Chimwenda ni meneja wa shirika la umeme tanesco wilayani hanang ambapo hapa anatoa maneno yake kwa wananchi pamoja na kuhakikishia wananchi kuwarejeshea huduma mara moja.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa manyara kamishina msaidizi Franci Masawe anadhibitisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio.
Kwa mujibu wa kamanda masawe majina ya watuhumiwa yanahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi.
No comments:
Post a Comment