Trending News>>

VILABU VYA ULAYA VIMEPINGA HOJA MPYA YA FIFA

Wakati hapa nyumbani Bodi ya Ligi ikisuasua kwenye baadhi ya maamuzi mhimu yenye maslahi kwa vilabu na taifa kwa ujumla huko Ulaya shirikisho la vilabu vya soka European Club Association (ECA), limeibuka na kupinga hoja ya FIFA ya kutaka kuongeza idadi ya timu kwenye Kombe la Dunia.

Jumla ya timu za taifa 32 huwa zinatunishiana misuli ili kumsaka bingwa wa dunia katika mchezo wa Kandanda, lakini mapema mwaka huu baada ya rais Gianni Infantino, kuingia madarakani aliwasilisha hoja ya kuongeza timu hadi 48 ifikapo mwaka 2026.

Hata hivyo, European Club Association (ECA), ambayo inawakilisha  zaidi ya klabu  200 imesema inapinga hoja hiyo ambapo imeeleza sababu kubwa ni kuongezeka kwa idadi ya mechi kwa wachezaji kitu ambacho hadi sasa bado wanafikiria namna ya kupunguza mashindano ili wachezaji wapumzike.

world-cup

“Bodi kuu ya ECA inakataa mpango huo na leo wamepeleka barua kwa Gianni Infantino wakiiomba FIFA kutoongeza idadi ya timu  katika Kombe la Dunia”.

Mwenyekiti wa ECA Karl-Heinz Rummenigge amesema: “Tuna upenda mchezo wa mpira wa miguu hivyo Siasa na biashara havipaswi kuwa kipaumbele pekee katika soka. “Kwa maslahi ya mashabiki na wachezaji, tunawaomba Fifa wasiongeze idadi ya washiriki kwenye Kombe la Dunia.”

Baraza la Fifa linatarajiwa kufikia uamuzi katika mkutano wake ujao mwezi Januari

No comments:

Powered by Blogger.