Trending News>>

UN kunoa vijana zaidi ya 30,000 nchini


UMOJA wa Mataifa nchini (UN) kwa mwaka ujao unatarajiwa kutoa mafunzo kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa vijana zaidi ya 30,000 hapa nchini.

Akizungumza wakati akifunga semina ya Fursa, jana, Dar es Salaam Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema semina za Fursa zimebadilisha maisha ya vijana wengi na hivyo ushirikiano wake na UN katika kufikia vijana utatoa nafasi ya vijana kuyaelewa malengo ya dunia.

“Vijana wengi wana ari ya kushiriki katika kufanikisha malengo ya dunia, ndio maana Umoja wa Mataifa umeamua kushirikiana na Fursa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanayafahamu malengo haya lakini pia wanashiriki katika kuyatekeleza na tumefurahi kupitia fursa tumeweza kuwafikia vijana zaidi ya 10,000 na kiwapatia mafunzo,” alisema Alvaro.

No comments:

Powered by Blogger.