Trending News>>

Steven Gerrard akamata kazi ya ukocha ndani ya Liverpool.

 Steven Gerrard ameanza vizuri na mchakato wake kuelekea kutimiza mawazo ya watu wengi sana ambayo ni kuiongoza Liverpool kama kocha. Baada ya kuiongoza Liverpool kama captain kwa muda mrefu sasa hivi mafanikio ambayo Gerrard anaweza kuyapata ni kuwa kocha bora hapo baadae.

Sasa hivi Steven Gerrard amepewa kazi ya kuwa manager wa academy ya Liverpool ambayo ilimtoa yeye mwenyewe na wakima Michael Owen, Robbie Fowler.

Klopp na uongozi mzima wa Liverpool unamuona Gerrard kama kocha wa Liverpool wa baadae. Ikiwa sasa anafanya kazi ya kuwakuza vijana wa Liverpool kuna uwezekano mkubwa baadhi yao akawaongoza hapo baadae kama akipata nafasi ya kuwa kocha.

Gerarrd alitangaza kustafu kucheza soka mwezi mmoja uliopita baada ya kucheza miezi 18 na L.A Galaxy inayoshiriki ligi ya Marekani.

Gerrard alipewa ofa ya mkataba na club ya A.C Milan lakini Gerrard mwenye miaka 36 aliamua kuchana nayo na kuanza maisha mapya ya ukocha.

No comments:

Powered by Blogger.