Trending News>>

Shinda safari ya Uingereza ukajiachie na Super Star mmoja kati ya hawa


Kampuni ya simu ya Tecno hii leo December 3 2016 imezindua kampeni ya Christmas ambayo inawawezesha wateja wake kujishindia tiketi za safari ya kuzuru nchini Uingereza katika kampeni inayokwenda kwa jina la #KamaMbele. Uzinduzi huu ni katika jitihada za Tecno kuwapatia wateja wake zawadi katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka Mpya na kuwawezesha kununua simu bora kwa gharama nafuu hivyo kuwawezesha kufurahia pamoja.
Katika kampeni hii mwanadada mrembo anayeng’arisha video za mastaa wa Bongo (Video Vixen), Hamisa Mobetto na mshindi wa Big Brother Africa – Hotshots mwaka 2014, Idris Sultan ni mabalozi wa kampeni hii ambapo mmoja wao kati ya  Idris au Hamisa atashinda safari ya Uingereza akiambatana na shabiki mmoja.
Hivyo ili mteja uweze kushiriki shindano hili  unatakiwa kuingia kwenye tovuti ya shindano ambayo ni http://tecnokamambele.co.tz/, utapiga kura kwa supar staa mmoja kati ya Idris au Hamisa kisha utaeleza kwanini unaikubali Tecno yako ukitumia hashtag #KamaMbele na shabiki mshindi atapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na mashabiki katika hatua ya pili ya shindano.
Mbali na kujishindia safari ya kwenda nchini Uingereza, wateja wa Tecno na Watanzania kwa ujumla wataweza kujishindia zawadi mbalimbali na kupata punguzo la bei katika simu za Tecno. Unaweza kutazama video hii kwa kuingia http://tecnokamambele.co.tz/, na kumpigia kura Idris Sultan uwe kwenye nafasi ya kuibuka mshindi wa Safari.

Vilevile kama Endapo utapenda kusafiri na Hamisa Mobeto, unaweza kutazama video hii kisha ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura.

Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno  kuweza kufahamu zaidi.
VIDEO: Tecno Phantom 6 Plus ilivyoanza kuuzwa, Wateja wataja kilichowavutia 

No comments:

Powered by Blogger.