Trending News>>

SORRY MADAM -Sehemu ya 3 & 4 (Destination of my enemies)


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Yule mshenzi amepewa uwaziri wa ulinzi Tanzania?”
“Mungu wangu………ana sifa gani za yeye kuwa waziri?”
“Ndio hivyo. Yaani laiti ningejua huyu mchenzi ningemuua tangu tukiwa ndani ya ndege ninaamini kwamba tusinge kuwa tunazungumza mazungumuzo ya kumuuhusu huyu kibwengo mtu”
“Kwa nini usimuue?”
“Mazingira hayakuruhusu, alipelekea kunipa shida ya kutafutwa hapo bendeni kwa hayati Mzee Madiba”
“Ulitokaje tokaje ndani ya ndege?”
Swali la Madam Mery likamfanya Mzee Godwin kurudisha kumbukumbu zake nyuma kwa haraka hadi siku aliyo toka kupambana na Eddy ndani ya ndege na taratibu akaanza kusimulia.

ENDELEA
“Nilipo onekanana sura yangu, iliniazimu mimi kuondoka na kuachana na Edddy kwani endepo ningeendelea kupambana naye ningeingia mikononi mwa askari na ingekuwa ni swala jengine.”
“Nilijichanganya katikati ya askari ambao walikuwa wakikagua watu basi, nikafanikiwa kutoka pasipo wao kugundua kwamba mimi ndio niliye kuwa nimesababisha maafa hayo”
 
“Sasa uliingiaje ndani ya ndege?”
“Ahaa, nilimtumia njia ya kujificha kwenye mizigo, baada ya kumuona Eddy akiwa anahangaikia usafiri wa kuja nchini Tanzania”
“Aiseee una hatari kweli kweli wewe”
“Weee acha tu, sasa lengo na thumuni la kukuita hapa ninahitaji kuweza kumpoteza Eddy mara moja kwenye huu uso wa dunia. Ila tahadhari ni moja, dogo amekuwa waziri, tena waziri wa ulinzi”
 
“Kama nilishindwa kumuua kipindi akiwa mtu wa kawaida, basi ujue kazi ya kumuangamiza yeye ni kubwa sana”
Madam Mery akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Mzee Godwin anaye onekana kuwa na mawazo mengi kichwani mwake. Mzee Gowin kabla hajaendelea kuzungumza ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake, taratibu akaanza kuusoma, na tabasamu pana likajijenga usoni mwake ikiwa ni ishara ya furaha
                                                                                         ***
    Kukamatwa kwa mchungaji Mandingo na Madam Glory watu maarufu katika nchi ya Tanzania kukaana kuwashangaza wananchi wengi, vyombo vingi vya habari vilidai kwamba watu hao wamekamatwa na waziri mpya wa ulinzi. Waandishi wengi walifunga foleni kwenye jengo la waziri wa ulinzi wakihitaji kufanya mkotano na waziri huyo ambaye hadi sasa hivi hawamuelewi nini ni maana ya kuwakamata watumishi hao wenye kumsaidia kila mwenye shida mbele ya macho yao
“Muhesimiwa, muheshimiwaa”
Waandishi baadhi walimuuita Eddy alipo kuwa akishuka kwenye gari lake.
 
“Ni kwa nini umeamua kuwakamata watumishi wa bwana Mchungaji Mandingo na Madam Grory?”
Muandishi mmoja wa gazeti la Habari Sasa alimuuliza waziri Eddy Godwin
“Siwezi kuzungumza lolote kwa sasa, ila huo ni mwanzo tu waujibikaji wangu, ila kazi inaendelea”
Eddy alijibu na kuomba kupishwa kukiwahi kikao cha wakuu wa jeshi la polisi ambao tayari wamesha wasili kwenye ukumbi wa mikutano tangu saa mbili asubuhi. Eddy hakuwa na haja ya kwenda ofisisni kwake moja kwa moja akaelekea katika ukumbi wa mkutano, Akawakuta wakuu wote wa jeshi la polisi, kutoka mikoani mwote wakiwa wanamngojea.
“Wakubwa zangu shikamoni”
 
Waziri Eddy alisalimia kwani watu wote waliomo ndani ya ofisi yake wamempita umri mkubwa sana na wengine ni sawa na baba zake. Kila mmoja akaitikia salamu hiyo
“Samahani kwa kuchelewa kuweza kuwahi kwenye kikao, ila hakuna kilicho haribika.”
“Lengo la kuwaita hapa ninahitaji kujadiliana nanyi, kuhusiana na watendaji wenu katika mikoa yenu.”
“Napenda kujua ni nini kilicho pungua kwenye idara yenu kuanzia madai munayo idaia serikali ili yaweze kulipwa haraka iwezekanavyo”
Eddy alizungumza na kuwatazama wakuu wote walio fika kwenye kikao hichi. Mmoja akanyoosha kidole na kuzungumza.
 
“Mkuu hapo kinacho tusumbua kwanza ni ufinyu wa mishahara kwa vijana wetu, mishahara kupungua na mazingira mabaya ya nyumba wanazo ishi kambini. Magari ni machakavu, piklikipi za doria ni chache kwahiyo inapelekea vitendo vingi vya uhalifu kufanyika katika nchi yetu”
“Asante nitalishuhulikia, mwengine”
“Muheshimiwa sisi tunahitaji sihasa isiingizwe kwenye majeshi kama hawa wezako walio pita kwa maana walikuwa wakituletea siaaa kwenye kazi zetu na kujikuta vijana wetu wakishindwa kufanya kazi kwa amani, jambo linalo pelekea uhalifu kuzidi kuongezeka”
 
“Asante baba yangu, ngoja niwatoe hofu kwenye hili. Mimi si mwana siasa na wala sina chama ila ninanchi. Labda nitoe rai moja kwenu. Musidanganyike na mwanasiasa yoyote. Yoyote ambaye ataingia kwenye jeshi la polisi, kama muhalifu hakikisheni munamuua na si kumuacha hai”
Wazo la waziri Eddy Godwin likawafanya wakuu wengi wa jeshi kushangaa kwani hawakutegemea kupata wazo kama hilo kwenye kikao hicho.
“Muheshimiwa kumbuka kwamba sisi ni jeshi la polisi kazi yetu ni kulinda wananchi na mali zao. Sasa unapo sema tuwaue inakuwa ni kazi kidogo kwetu huoni kwamba tutakuwa na sifa mbaya?”
 
“Samahani baba yangu kwa majibu haya nitakayo kupa, ila kiukweli hadi sasa hivi nyinyi muna sifa mbaya mbaya mbaya zaidi ya shetani na ubaya wake. Wahalifu wengi tupo nao huku juu serikalini. Wanawatumikisha vijana wadogo wanakamatwa na kufungwa, ila muzizi ipo inaendelea kuzalisha matatizo mengine mengi kwenye ngi hii. Sasa hii ni amri wala sio ombi, na lolote litakalo fanyika basi mimi nitakuwa muwajibikaji katika kuyajibu hayo ICC”
Baadhi ya wakuu wa polisi wakapiga makofi kwa ujasiri anao uonyesha kijana mdogo mwenye mamlaka makubwa kwenye nchi hii.
“Tumekuelewa muheshimiwa”
“Asanteni kwa kunielelewa, ila wapeni tahathari vijana wenu. Nitakuwa nikizunguka zunguka kwenye kila mkoa na vituo vyote kisiri pasipo wao kujua, endapo nitaumdua kuna ubadhilifu wowote kwa wananchi basi, kijana huyo au hao watawajibika katika hilo. Asanteni kwa muda wenu”  
 
***
“Mbona unatabasamu?”
Madam Mery alimuuliza mzee Godwin
“Kijana wangu, niliye potezana naye muda yupo hai”
“Ni nani?”
“John”
“John yupi?”
“Yule aliye kua mwanafunzi wako”
Furaha ya mzee Godwin na Madam Mery ikazidi kuongezeka kwani mtu waliye kuwa wanamtegemea kwenye mipango yao wamepata ujumbe wake kwa njia ya simu.
“Sasa yupo wapi?”
“Yeye mwenyewe hakuniambia kwamba yupo wapi ila atanijulisha kwamba yupo wapi”
“Sawa”
“Ila itabidi kuunda kikosi chenye nguvu na safari hii, Eddy nilazima afee”
Mzee Godwin alizungumza huku akiachia tabasamu pana usoni mwake, macho yake akiwa amemtazama Madam Mery.
                                                                                         ***
“Mume wangu huoni kama unalo lifanya ni jambo la hatari kuwakamata hao watumishi wa Mungu”
Phidaya alizungumza kwa saut ya unyonge huku akimuandalia mumewe chakula cha usiku
“Haiwezi kuwa hivyo mke wangu, na wale si watu wa Mungu kama munavyo dhani nyinyi ni waovu sana”
“Wamefanya nini watu wa watu?”
“Wale ndio wanao jihusisha na mauaji ya walemavu wa ngozi na kuingiza madawa ya kulevya nchini”
“Wewe umejuaje?”
“Wao wenyewe wanadai hilo, ila uchunguzi unaendelea kufanyika mambo yakiwa sawa nitakujulisha”
“Mmmm ila kua makini mke wangu nisinge penda kuona unarudi kwenye matatizo kama ilivyo kua awali”
Phidaya alizungumza huku akimsogelea mume wake na kumkumbatia mumewe anaye onekana kutawaliwa na mawazo mengi baada ya kazi ngumu, 
 
“Shamsa yupo wapi?”
“Yupo ndani amelala”
“Nenda kamuite. Ninamazungumza naye kido”
Phidaya akanondoka na kupandisha ngazi za gorofani na kwenda chumbani kwa Shamsa, akamkuta Shamsa akiwa anasoma kitabu cha My Mommy’s friend.
“Bado hujamaliza kusoma kitabu chako?”
“Ahaaa bado hichi kitabu kimenichanganya”
“Kwani amekiandika nani?”
“Jamaa mmoja anaitwa Eddazaria Gershom Msulwa”
“Haya weka pause baba yako anakuhitaji yupo chini, huko anakula”
Shamsa akaongozana na Phidaya hadi alipo Eddy, wakamkuta akiendelea kula taratibu huku mawazo mengi yakiendelea kukitawala kichwa chake
“Vipi umefanya kazi ile nilioyokuagiza?”
Eddy alizungumza kwa sauti iliyo jaa uchovu mwingi.
 
“Kazi ipi baba?”
“Ile ya kutafuta chuo cha udaktari?”
“Ndio baba, ila bado hadi sasa hivi sijapata chuo kizuri”
“Basi kesho nitaulizia ofisini, je india si unaweza kwenda kusoma?”
“Ndio baba”
“Poa, basi wewe jiandae muda wowote nikipata chuo ukusanye virago ukasome”
“Sawa baba”
Shamsa  akaondoka akiwa na furaha sana moyoni mwake kwani ni moja ya ndoto zake kuja kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya wamama na watoto.
Eddy akamaliza kula na kuingia ndani kwake na kujitupa kitandani, usingizi mzito ukampitia.
 
   ***

   Siku zikazidi kukatika huku hofu kubwa ikaanza kutawala katika vikundi vya majambazi ambao mara nyingi waliweza kuyafanya matukio yao kwa kujiamini sana, wakiamni kwamba wapo baadhi ya wakuu wa serikali wanaweza kuwatetea, pale wanapo kamatwa. 

Mfano ukaanza kwa majambazi walio teka gari la abiria katika mkoa wa Kagera, Kwa bahati mbaya au nzuri, gari ya polisi iliweza kufika katika eneo la tukioa ambapo wakafanikiwa kuwatia nguvuni majambazi wanne. Kutokana na agizo la waziri wa ulinzi Eddy Godwin, majambazi wote walipigwa risasi za kichwa mbele ya abiria walio kuwa wametekwa, ikiashiria kwamba jeshi la polisi lilianza kufanya kazi yake kama ilivyo paswa kufanya.
 
Taratibu wananchi wakaanza kurudisha imani zao katika jeshi la polisi, huku wakianza kumsifu kichini chini waziri wa ulinzi ambaye kwa mara ya kwanza walihisi atakua ni mbabaishaji kwao.
Utendaji kazi wa waziri mpya bwana Eddy Godwin, ukaanza kuzua mtafaruku kwenye bunge, huku baadhh ya wabunge wali,subiri kwa hamu, mbunge huyo kwenye kipindi cha maswali na majibu, ambacho kimeanza leo,
“Mke wangu, leo nipo kikaangioni naomba uniombee”
Eddy alizungumza kwa kupitia simu akiwa ndani ya chumba cha hoteli aliyo fikizia mjini Dodoma
“Upunguze hasira kwa maana ninavyo kujua wewe, unaweza kumng’oa mtu meno”
 
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ipole iliyo jaa usingizi mzito kwani ni alfajiri na mapema aliweza kuanshwa na mlio wa simu iliyo pigwa na mimewe.
“Siwezi mke wangu, unajua tangu nimepewa haya madaraka nimejikuta nikiwa mstaarabu sana”
“Sawa mume wangu, mimi nakutakia kila la heri katika hilo”
“Asante mke wangu”
“Alafu nilikua nimesahau kukukumbusha, Shamsa leo anaondoka na ndege ya saa tisa alasiri kwenda India”
“Ahaaa, hata mimi nilikua nimesha jisahau. Lakini si kila kitu mumesha kikamilisha?”
“Ndio”
“Junio bado yupo kwa bibi yake?”
“Ndio, jana nimekwenda kumchukua kakataa kata kata yaani sijui nitaishije peke yangu kwenye hili jumba”
“Usijali mke wangu, nikipata nafasi nitachomoka mara moja kuja kukuona, Au unweza kwenda kukaa kwa mama kama unaogopa”
 
“Sawa mume wangu, nakupenda sana”
“Nami pia ninakupenda”
Phidaya akambusu Eddy kama mazoea waliyo yajenga kwenye mahusiano yao, pale wanapo kua wakiwasiliana kwa simu, mmoja wao anaweza kuanza kumbusu mwenzake, Eddy taratibu akanyanyuka kitandani, akaingia bafuni na kuoga kisha akarudi chumbani, akafungua kabati alilo weka suti yake ya kuvaa siku hiyo, akaivaa taratibu hadi akamaliza. Akaweka kila kitu chake sawa. Kisha akampigia simu mzee Selemani Mbogo, ajitayarishe kwa safari ya kuelekea bungeni/
 
“Mimi mbona nipo tayari, mwanangu ninakusubiria wewe tu”
“Sawa ninakuja baba yangu”
Eddu a;ipo hakikisha kila kitu amekiweka sawa, akatoka chumbani kwake na moja kwa moja akaelekea mapokezi ambapo akakutana na askari anaye mlinda, na wote kwa pamoja wakeelekea kwenye gari. Haikuchukua dakika nyingi wakawa wamefika bungeni, tayari waandishi wa habari wa mashirika mbalimbali wakamvamia kumuhoji maswali mawili matatu.
 
“Una lipi la kuwaambia wananchi juu ya ulinzi wao na mali zao?”
Muandishi wa gazeti la FURAHA LEO, aliuliza
“Ulinzi unaendelea kuhimarika kikubwa ninawaambia wasiwe na mashaka na jeshi zima. Asanteni ninawahi ndani”
Eddy kwa msaada wa askari anaye mlinda akaondoka mikononi mwa waandishi wa habari na kufanikiwa kuingia ndani, ya bunge moja kwa moja akelekea kwenye kiti chake kilichopo karibu sana na sehemu ya kujibia maswali atakayo ulizwa na wabunge wezake pamoja na mawaziri. Kama ilivyo kawaida ya wabunge kusimama pale anapo ingia spika wa bunge, akafika kwenye kiti chake ambapo, akasoma sala ya kuliombea taifa kwa ujumla pamoja na bunge tukufu, kisha shughulii za kibunge zikaanza.
 
Macho na masikio ya wananchi wengie waliyaelekeza kwenye, televishion pamoja na redio zao kuweza kusikia kitakacho jibiwa na waziri huyu mpya ambaye utendaji wake wa kazi ni tofauti sana na mawaziri wengine ambao, wamepita kwenye sekta yake ya ulinzi. Waziri Eddy Godwin akaanza kusoma taarifa fupi kuhusiana na wizara yake tangu aweze kuachiwa madaraka na waziri aliye pita.
 
“Muheshimiwa spika, wizara yangu ya ulinzi, hadi sasa hivi utendaji wake umekua ni mzuri japo bado tunaendelea kufanyia kazi baadhi ya maeneo ikiwemo, kuendelea kuwalipa watumishi wa jeshi la polisi madai ya mishaara yao ambayo, hadi ninaingia madarakani, walikua wakiidai serikali kiasi cha shilingi bilioni kumi na nusu.”
 
“Pesa hizo hadi leo nimeweza kukabidhiwa shilingi bilioni mbili tu, huku nikiambiwa kuweza kusubiri mwaka wa serikali uweze kufika jambo ambalo inaonyesha kuna ukiritimba unao endelea ndani ya serikali hususani kwenye sekta ya fedha, Labda niseme kitu kimoja kwenye serikali yangu tukufu. Sinto mfumbia macho kiongozi yoyote awe ni raisi au nani, endapo nitabaini kwamba anahusika kula ela ya uma na kuwapa shida watendaji wadogo, basi nitahakikisha sheria inachukua mkondo, Asanteni”
 
Risala ndogo ya waziri Eddy Godwin, ikawastua baadhi wa viongozi, kwani tayari wamesha anza kuziona cheche za kijana huyo ambaye ni waziri aliye chaguliwa na muheshimiwa raisi bwana Praygod Makuya.
“Nakaribisha maswali na majibu”
Spika wa bunge akatoa nafasi kwa mbunge wa viti maalumu kuweza kuuliza maswali yake kwa waziri wa ulinzi bwana Eddy Godwin.
“Muheshimiwa spika swali langu la kwanza kwa huyu waziri mpya, Je anasifa za kuingia humu bungeni na kukabidhiwa wizara hiyo. Pili mbona kama amerithishwa kutoka kwa waziri mkuu aliye pita, tatu umri wake ni miaka mingapi? Asante muheshimiwa naibu spika”
Macho ya Eddy yakamtizama mama huyo aliye zungumza kwa asauti kali akionyesha dhahiri amejenga chuki dhidi yake,
“Laiti ningekua si waziri, ningekushushia matusi hadi ujisikie vizuri”
Eddy alijikuta akiropoka pasipo kuzima kinasa sauti chake(maiki), Jambo lililo wafanya watu wengi kushangaza na hiyo kauli.
                                                                                            SORRY MADAM(4)  (Destination of my enemies)

Eddy akajikuta akimtazama mama huyo kwa hasira kali kwani maswali aliyo yauliza hayakuwa na tija yoyote kwake, isitoshe swali lililo mkera zaidi ni lile la kuambiwa kwamba ameridhishwa uongozi huo kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa ni waziri mkuu wa Tanzania. Kamera zaote za vyombo vya habari vilivyo kua ndani ya bunge, vikamuelekea Eddy, huku baadhi ya makamera man, wakiivuta sura ya Eddy akiwa amekasirika, gafla hali ya Eddy ikabadilika na kuachia tabasamu pana, lililo mfanya mke wake Phidaya kushusha pumzi kubwa kwani anamuelewa vizuri sana mume wake akiwa amekasirika.
 
“Nianze kukujibu hivi, Moja sina sifa ya kuongoza wizara hii, kwasababu mimi sio mwama siasa ila nina uwezo wa kuiongoza kwa sababa ninajua nini ninafanya.”
“Mbili umri wangu haukuhusu, kwani kwa uzee wako wewe mama, ila unaonekana una akili ndogo kama mtoto wa chekechea.”
“Tatu, sijaridhi uongozi, ila raisi wangu mtukufu ndio ameniteua kuchukua hii nafasi baada ya wanasiasa wezako kushindwa, Asante”
Majibu ya Eddy yakepelekea wabunge baadhi kupiga makofi kwenye meza zao ikiashiria kwamba wamependezwa na majibu yake huku baadhi yao wakionekana kukasirishwa na majibu hayo ya kebehi kutoka kwa kijana mdoho huyo.
“Muhesimiwa muongozoo”
 
Mbunge mmoja alizungumza pasipo kuruhusiwa na spika wa bunge, ikamlazimu spika wa bunge kumruhusu mbunge huyo.
“Muheshimiwa spika, katika kifungu cha maadili mwaka 1979 namba 11, kina sema hivi ninanukuu. Si ruhusa kwa mbunge yoyote au waziri kutoa lugha ya kudharau mwengine, akitokea mmoja wapo akakiuka hilo basi inampasa aweze kuomba radhi. Mwisho wa kunukuu. Tunamuomba waziri wa ulinzi kuweza kuomba Radhi kwa kumdharau mbunge wa viti maalumu kwa kumlinganisha akili zake kama mtoto wa chekechea.”
 
Mbunge huyo akakaa kwenye kiyi chake na kuwafanya wanao muunga mkono katika hilo kuweza kupiga madawati yao na kuifanya sauti ya madawati yao kuizidi sauti ya walio muunga Eddy kwa majibu yake.
“Waziri wa ulinzi, unatakiwa kuomba Radhi kwa lugha hiyo”
Spika wa bunge alizungumza huku akimtazama Waziri Eddy Godwin katika sehemu aliyo simama.
 
“Mungu wangu…..!!! Kwa bahati mbaya mumekosea sana kutamka swala la mimi kuomba radhi, ninasema hivi siwezi kuomba radhi kwa mshenzi mmoja ambaye yeye na wezake humu ndani wanajihusisha na uuzaji  wa madawa ya kulevya, ufisadi na mambo mengine. 

Hembu ngoja niwaambie kitu kimoja mimi sio mwana siasa na hakuna ambaye anaweza kunifanya chochote kutokana ninasimama kwenye sheria ya kuwatetea wananchi na walala hoi ambao maisha yao yanazidi kua magumu kutokana na wajinga wachache kama huyo mama na huyo mwehu mwengine aliye nitaka mimi kuomba radhi, musahau juu ya hilo swala na wale wote ambao wanajijua wana mijidudu yao wanaifanya huko nje wajiweke tayari kwani vita imeanza, nitamkamata mmoja baada ya mwengine. Asanteni”
 
Ukumbi mzima wa bunge ukatawaliwa kwa fujo za maneno, ya baadhi ya wabunge ambao walihisi wametukanwa na kijana huyu mdogo, huku wengine wakionekana kushangilia kwa ujasiri ambao ameuchukua kijana huyo ambaye ni mpya kuingia kwenye bunge hili tena akiwa na cheo cha waziri wa ulinzi.
 
“Jamani waheshimiwa wabunge ninaomba mutulie”
Spika wa bunge akawa na kazi ya ziada kuweza kuwanyamazisha wabunge hao kutulia, Eddy hakubanduka kwenye sehemu aliyo simama, macho yake yakawa na kazi ya kuwatazama wabunge walio nyanyuka akiwemo aliye muhitaji aweze kuomba radhi, akionekana akiwa na jazba kubwa sana akitamani kushuka kwenda kumtandika Eddy pale alipo kwani anamfananisha na mwanaye wa mwisho kabisa. Spika wa bunge akafanikiwa kutuliza ghasia hizo zilizo zuka gafla bungeni.
 
Wananchi walio sehemu mbali mbali, wakajikuta mioyo yao ikizidi kumpenda waziri Eddy ambaye anaonekana kuwa yupo tofauti sana na viongozi wengine
“Aisee chalaa wangu, tungepata mawaziri kumi kama hawa, ninaimani nchi ingenyookoa hii”
Alisikika mchaga mmoja akiropoka katikati ya walevi ambao, wanaendelea kuburudika na unywaji wa pombe ya mbege mapema hii na asubuhi.
“Tunaendelea na maswali”
“Asante sana muheshimiwa spika, kwanza ningependa kumpongeza muheshimiwa Eddy kwa majibu yake, kusema kweli ni viongozi wachache ambao wanaujasiri wa kujibu kama alivyo jibu bwana Eddy. Kusema kweli muheshimiwa Eddy wewe kaza buti achana nao hawa walanguzi wa mali za uma, langu ni hilo kaka”
 
Mbunge mwengine ambaye anaonekana ni kijana, alijitoa muhanga kumsifia Eddy ambaye kwa muda mchache umaarufu wake, ukazidi kuongezeka kwenye mitandoa mingi ya kijamii, huku picha zake zikiwekwa kwenye mitandao kama facebook, twitter, jamii forams, whatsapp na kadhalika, huku kukiwa na maandishi kwenye picha yeki yanayo sema. (“UNAAKILI NDOGO KAMA MTOTO WA CHEKECHEA)
Amani ikazidi kutoweka kwa baadhi ya viongozi ambao, wanamambo ambayo ni kinyume na maadili ya kazi zao. Kila mmoja akaanza kutuma ujumbe wa simu kwa watu wanao shirikiana nao ambao si viongozi wakiwaomba waweze kua makini kwani hali ya kazi zao hizo ipo hatarini.
 
{MUHESHIMIWA USIWE NA SHAKA HIZO NI NGUVU ZA SODA}   
Meseji moja ikaingia kwenye simu ya mbunge mmoja ambaye alikua akiendelea kusikiliza majibu na maswali ambayo anaendelea kuyatoa waziri Eddy Godwin. Msisimko wa bunge ukazidi kuongezeka, kwa wananchi ambao mara kwa mara walisikika wakimzungumzia Eddy ambaye anaendelea kuwapasha baadhi ya wabunge.
“Natoa agizo kwa jeshi la polisi kuanzia kesho, wahakikishe kwamba baa zote zinaanza kufanya kazi kuanzia saa tisa jioni, watakao kiuka agizo hatua za kisherika zichukuliwe, Asanteni”
 
Eddy akamalizia kwa kutoa agizo na kuwafanya wabunge wanao muunga mkono kumpigia makofia ya kumpongeza huku wanao mchukia wakikaa kimya. Bunge likahairishwa hadi jioni na wabunge wote wakapata muda wa kwenda kupumzika. Waandishi wa habari wakajiandaa kwa kuweza kumuhoji maswali waziri Eddy huku swali  lao kubwa wakihitaji kumjua ni nani anaye jihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya,
 
“Bado mapema sana, ila watakua hadharani hivi karibuni, naombeni nikapumzike nijiandae kwa kikao kijacho”
Eddy akaondoka na kuingia ndani ya gari lake. Wakarudi hotelini walipo fikizia moja kwa moja akaelekea chumbani kwake huku akiwa na askari anaye mlinda, baada ya kuufungua mlango akaingia askari wake na kukikagua chumba kisha akamruhusu Eddy na yeye kuingia ndani ya chumba hicho kisha askari huyo akatoka nje. Eddy akajiputa kitandani huku akionekana akiwa amechoka sana kwa shuhuli nzima ya kujibu maswali  ambayo mengine hayakumuhusu yeye ila kutokana yupo kwenye wizara hiyo ilimpasa kuweza kuyajibu kikamilifu.
“Hii kazi kweli ngumu mmmmmm”
Alizungumza huku akiwa amejilaza kitandani, akiwa anaendelea kujizungusha zungusha kitandani, ili kuupumzisha mwili wake, simu yake ikaita akaitoa mfukoni, na kukuta namba ngeni ikiwa inaita, akaipokea na kuiweka sikioni taraibu.
 
“Habari”
Eddy alinza kumsalimia mtu huyo aliye mpigia simu hiyo.
“Hahahahaa, Eddyyyyyyy. Wewe pia ni jasiri kama mama yako si ndio?”
Sauti ya mzee Godwin ilisikika upende wa pili wa simu jambo lililo mstua sana Eddy kwani hakutegemea kusikia sauti ya baba yake huyo ambaye ni adui yake nambari moja
“Naamini kwamba, utakua unajiuliza namba yako nimeitoa wapi, ila usijali ni swali dogo sana hilo, na jibu lake namba yako amenipa mwanangu…..”
“Mwanao nani?”
Eddy aliuliza kwa sauti ya ukali, iliyo mfanya mzee Godwin kuangua kicheko cha dharau
                                                                                                    ***
    Kazi ambayo walianza kuifanya Mzee Godwin na Madam Mery ni kuweza kuchunguza ni wapi anapo ishi Eddy, ikawalazimu kufunga safari hadi  nchini Tanzania wakitumia basi wakitokea Nairobi nchini Kenya, ambapo walipitia mpaka wa horohoro uliopo Tanga, moja kwa moja wakafika Tanga mjini, ambapo kwa kutumia basi wakaweza kufika jijini Dar es Salaam, wakachukua chumba katika holel ya HOLDAY INN, na taratibu wakaanza kufanya upepelezi wa kugundua ni wapi anapo ishi Eddy.
 
Haikuwa ni kazi ngumu sana kwao kuweza kupatambua anapo ishi Eddy, hii ni kutokana na jina lake kuzungumza sana midomoni mwa watu wali wengie wakiukosoa uteuzi wa raisi bawa Praygod Makuya juu ya kiongozi huyu Eddy. Siku walio weza kupafahamu nyumbani kwa Eddy ni siku ambayo Eddy, yupo bungeni kwenye kipindi maalimu cha maswali na majibu, dereva taksi mmoja aliweza kuwapeleka nyumbani kwa Eddy bwana Godwin na Madam Mery.
 
“Nyinyi ni kina nani?”
Askari anaye linda geti la Eddy alimuuliza Mzee Godwin kimashaka, kwani sura ya mzee Godwin, inaendana sana na sura ya bosi wake Eddy
“Hivi ukinitazama unahisi mimi ni nani kwa Eddy?”
Mzee Godwin, alijibu kwa mtindo wa kuuliza swali kwa askari huyo, aliye bakia akimtazama Mzee Godwin, kwa umakini. Taratibu akajikuta akifungua geti na kuwakaribisha mzee Godwin na Madam Mery. Pasipo kuwakagua kwa kifaa maalumu ambacho hukitumia kumkagua kila aingiaye ndani ya jumba hilo la kifahari.
 
“Wenyewe wapo?”
“Yupo tu mama, twende niwapeleke”
Askari huyo alizungumza huku akitangulia kwenda sehemu alipo kaa Phidaya, kwenye moya ya kibanda cha kupumzikia chenye Tv kubwa, akiendelea kufwatilia bunge hilo, akimshuhudia mumuwe jinsi anavyo jibu maswali kwa kujiamini. Hatua chache mbeleni, Mzee Godwin akatoa bastola yake pasipo askari kugundua lolote, kwa nguvu akapiga askari kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki na kumfanya aanguke chini mzima mzima na kuzimi.
“Mbona hivi….!!?”
Madam Mery alilishangaa tukio hilo la mzee Godwin, kumfanyia askari huyo.
 
“Najua nini nafanya”
Kutokana walisha kiona kibanda alicho kaa Phidaya, ambaye akili na mawazo yake yote ameyepeleka kwenye bunge hilo, hakulishuhudia tukio la askari wao kupigwa. Mzee Godwin na Madam Mery wakafika sehemu alipo kaa Phidaya.
“Habari”
Madam Mety alianza kumsalimia Phidaya na kumfanya astuke, baada ya kumuona mzee Godwin akikaa kwenye kiti cha karibu yake, huku mkononi mwake akiwa ameshika bastola.
“Mwanangu amejitahidi sana, ameoa shombeshombe”
Mzee Godwin alizungumza huku akizishika nywele ndefu za Phidaya na kuzisogeza puani mwake na kuzinusa
 
“Mmmmmm, zinanukia marashi mazuri sana”
Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kebehi, iliyo zidi kumuogopesha Phidaya ambaye hakujua afanye nini kwa wakati huo, na laiti ange dhubutu kunyanyua kinywa chake, labda ungekua ndio mwisho wa maisha yake.
“Bunge limeisha, badilisha chaneli”
Mzee Godwin alizungumza huku akimpa rimoti Phidaya, ambaye mwili mzima unamtetemeka kwa woga. Madam Mery muda wote akawa na kazi ya kumdhaminisha Phidaya kuanzia chini hadi juu, huku akiwa haamini kwamba Eddy, ameweza kumiliki mwanamke mwenye vigezo vyote kuanzia chini hadi juu.
 
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”   
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simu yake aliyo kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga namba hiyo.    

==> ITAENDELEA

No comments:

Powered by Blogger.