Trending News>>

SORRY MADAM -Sehemu ya 1 & 2 (Destination of my enemies)


MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Televishen pamoja na Tv zote nchini Tanzania, zipo hewani, kuweza kuyanyakua mazungumzo ya moja kwa moja ya Raisi Praygod Makuya, kwenye uteuzi wa mawaziri wapya, hii ni kutokana na waziri mkuu kuweza kujiudhulu, kwa kusumbuliwa na matatizo ya kiafya yaliyo mchukua kipindi kirefu kukaa nje ya ofisi pasipo uwepo wake. Kama kanuni na taratibu za nchi ya Tanzania, inamlazimu raisi kuweza kufanya hivyo punde tu waziri mkuu anapokuwa ameachia kiti hicho kinacho tamaniwa na kila kiongozi aliyopo serikalini.
 
Raisi akaanza kutaja majina ya mawaziri wapya watakao chukua nafasi za mawaziri walio punguzwa kwenye wizara mbalimbali. Masikio ya wananchi wengi wa Tanzania, ni kwenye wizara ya ulinzi, ambayo katika siku za hivi karibuni imetokea kuyumba, hadi wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na jeshi zima la polisi. Majina kadhalika ya mawaziri wapya na wazamani walio badilishwa wizara ya kaendelea kutajwa, ikafikia kwenye wizara ya ulinzi ulinzi, hapa raisi akanyamaza kidogo na kumeza fumba la mate huku akizikodolea kamera zilizopo mita chache kutoka katika sehemu aliyo simama.
 
“Katika wizara ya ulinzi, nimeweza kufanya mabadiliko makubwa sana, ambayo ninaamini yatakwenda kufurahiwa na wananchi walio wengi. Kwa maana katika kipindi changu cha utawala nimeweza kupokea malalamiko mengi sana kuhusiana na uhalifu katika jamii inayo tuzunguka.”
“Wizara hii nimeweza kuweka watu hodari, wanao weza kuhakikisha wanafuta hofu yote iliyo jengeka katika mioyo mingi ya wananchi”
 
“Basi hapa waziri wa wizara hii, anaitwa Eddy Godwin, makamu wake atakuwa Bernad Ngoswe”
Wananchi wengi wakabaki wakiwa wameshangazwa na jina hilo kwani, hawajawahi kulisikia kwenye serikali tangu raisi Praygod kuingia madarakani.
“Hivi huyo Eddy Godwin ni nani?”
Mchaga mmoja alisikika akiwauliza wezake walio kusanyika katika duka lake la kuuza tv, redio na vitu vingine vya majumbani, lililopo maeneo ya Kariakoo.
“Hata mimi simfahamu”
“Hawa watakuwa wanagawiana, kwanini wasimpe yule….yule nani….”
“Chande?”
“Hapana yule, ambaye wamekwenda kumtupia kwenye kilimo”
 
“Ahaaaa Masele”
“Ehee huyo huyo, yule jamaa anaonekana yupo fiti sana”
“Yaani wee acha. Ila baadaye si wanaapishwa, tutakuja kumcheki huyo jamaa mwenyewe”
“Etieee”
“Naye asije akatuletea ufala kama huyu mwenzie aliye pita Haki ya Mungu, naye tutamuombea mabaya”
“Hahaaa maswawe punguza munkari bwana”
“Sio munkarti chalii yangu, yaani waziri akiwa ovyo hata hawa watendaji wake huku chini wote wanakuwa mambumbu,  hembu nenda pale sentral kaseme unatatizo uone kama hawata taka rushwa”

Nazungumzo ya watu mbalimbali katika mitaa tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam, yalikuwa ni kuhusiana na huyo waziri mpya waliye msikia jina lake likitajwa. Wengi wao hawakuonyesha imani yoyote kwa waziri huyo, wanaamini naye atafanya madudu kama aliyo yafanya waziri aliye pita, kwa kuweza kuwapa polisi, uhuru ulio ptiliza, hadi inafikia hatua kwamba wananchi wa maisha ya chini wananyimwa haki zao za msingi, na wenye pesa ndio waliweza kupata haki zao na kuwakandamiza wale wasio kuwa nacho.
                                                                                            ***
“Mume wangu utaweza, au ndio majukumu mazito uliyo kabidhiwa?”
Phidaya alimuulimuuliza mumewe, huku akimfunga tai vizuri kwenda kwenye sherehe ya wao kuapishwa inayo fanyikia kwenye viwanja vya ikulu muda wa jioni ya siku hii,waliyo tangazwa kama mawaziri wapya.
 
“Mungu ni mwema nitaweza tu”
“Eddy mume wangu usije ukaenda ukaboronga huko ikawa ni mamatizo, mengine. Napenda tuishi kwa amani”
“Baby wewe ndio mtu wa kunipa mimi moyo, ila si mtu wa kunikatisha tamaa”
“Sio kama nakukatisha tamaa mume wangu, kumbuka kwamba tumepitia shida nyingi sana, hadi leo tumepata hii amani, ninaona kwamba tutaipoteza amani hii”
“Never, nitahakikisha amani ya familia yangu kwanza, haiyumbi kisha nitahakikisha imani ya wananchi wangu, pia inapatikana”
“Sawa mume wangu mimi ninakuombea kila laheri, ila usisahau kwamba ninakupenda sana Eddy wangu, kupota maelezo”
“Nakupenda pia mke wangu”
Taratibu Phidaya akambusu mume wake mdomoni, akamuweka vizuri koti la suti aliyo ivaa. Wakatoka nje ya chumba chao na kuanza kushusha ngazi za gorofani hadi wakafika sebleni, walipo wakuta Shamsa na Junio wakitazama tv.
 
“Badilisheni chaneli muda si mrefu mutaniona nikiwa nimetokelezea kwenye kideo, nitaringaje”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka na kuwafanya watoto wake wote kucheka.
“Mungu wangu…!! Hapa hawajapata waziri”
Phidaya alizungumza huku akicheka kicheko, kilicho mfanya hadi machozi ya furaha kumwagika.
“Weee, waziri wameupata, yaani varangati nitakalo kwenda kulianzisha ni kama shehe aliye lishwa nguruwe pasipo kujua, sasa akagundua, hiyo movie yake nitawaadisia nikirudi”
“Hembu nenda huko muda ujue unakwenda, ngoja uvuliwe huo uwaziri wako uone kama utazunguka zunguka tena”
“Nani anivue, subutuu nitampiga ngumii moja tuu, hadi aimbe haleluya”
 
“Dady usisahaku kuniletea zawadi?”
“Mwanangu, huko ikulu kuna zawadi gani”
“Eddy nenda bwana unachelewa, weee jizungushe zungushe kama tiara”
Eddy akambusu mke wake, akafungua mlango na kutoka nje na kumkuta dereva wa gari la serikali akiwa anamsubiria kwa ajili ya kumpeleka ikulu kwenye sherehe hiyo.
“Shikamoo muheshimiwa?”
Eddy hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kuingia ndani ya gari na dereva huyo naye akaingia ndani ya gari, akawasha gari taratibu wakatoka kwenye geti kubwa la jumbu hili la Eddy alilo linunua siku chache baada ya kutoka katika mapumziko ya harusi yao yeye na mke wake Phidaya.
 
“Samahani ndugu yangu”
“Bila samahani muheshimiwa?”
“Wewe una miaka mingapi?”
“Arobaini na tano”
“Sasa mbona umenisalimia, wakati mimi bado kijana mdogo hata miaka thelethini bado sijainusa”
“Ahaa ujajua shida hizi mdogo wangu, ndio zinazo pelekea haya yote kutokea”
“Ahaaa basi, kuanzi leo nitakuwa ninakusalimia mimi, hata kama mim ni bosi wako. Naanza kwa kusema Shikamooo bwana nani…….”
“Selema Mbogo”
“Ahaa itikia basi salamu yangu, au hutaki”
“Marahabaa. Unajua pale nilivyo ona hujaitikia salamu yangu nikahisi kwamba ni mtu ambaye hupendi mazoea na mtu, kumbe ni mcheshi kiasi hichi”
“Kaka Mbogo, yaani mimi ni mcheshi sana, huwa sipendi kumkera mtu, hata kama nina kitu chochote kwenye maisha yangu”

Mazungumzo yao yaliendelea hadi wakafika ikulu, wakaruhusiwa kupita na kuingia, dereva akasimamisha gari kwenye maegesho yaliyopo hapo ikulu. Eddy akashuka na kupokelewa na wadada walio wekwa kwa kazi hiyo ya kuwapokea wageni wanao wasili kwenye viwanja hivyo, na moja kwa moja akapelekwa hadi kwenye viti maalumu walivyo andaliwa mawaziri wanao apishwa kwenye sherehe hizo. 

Karibia vyombo vyote vya habari nchini Tanzania, wakawa wameweka kambi ikulu, ili kuweza kurusha matangazo hayo yanayo ruka moja kwa moja kutokea ikulu.
Karibia viongozi waliopo ndani ya serikali macho yao mara kadhaa wakawa wanayatupia kwa Eddy, ambaye anaonekana ni kijana mdogo kupita viongozi wengine wote waliopo katika viwanja hivi
 
“Huyu si yule kijana wa waziri mkuu?”
Mzee mmoja alimuuliza mwenzake huku wakiwa wememkodolea mimacho Eddy
“Ndio huyu”
“Si alikufa, au emefufuka?”
“Mimi wala sijui mwenzangu, ila mama yake  si yupo tutamuuliza kimetokea nini”
“Ila huyu kijana wala sidhani kama anastahili kuwa kiongozi kwenye wizara ya ulinzi”
“Watakuwa wamepeana peana tu”
Maneno yote waliyo kuwa wanazungumza wazee haya Eddy aliyasikia vizuri, ikabidi awageukie na kuwatazama, nao wakajikausha na kujifacha kama si wao walio kuwa wakizungumza maneno kama hayo, mbaya zadi ni miongoni mwa mawaziri walio pigwa chini kwenye wizara walizo kuwa waklizitumikia kiuvivu uvivu. Eddy akatabasama na kuwakonyeza kisha akageukia mbele.
 
“Huyu mtoto mpumbavu kweli, anaonekana ana dharau sana”
“Anatukonyeza sisi, tumekuwa mademu zake”
“Ngoja tutamuonyesha, anadhani hii serikali ni rahisi kama anavyo fikiria na akili zake za asubuhi”
Eddy alibaki kucheka, kwani maneno wanayo yazungumza wazee hao yanaonekana ni maneno ya wakosaji kwani walipewa nafasi na wakashindwa kuzitumia katika muda muafaka.
 
Haikuchukua muda, raisi akaanza kazi ya kuwapisha mawaziri wake wapya ambao aliwateua majira ya asubuhi na kuwatangazia taifa kwa kupitia vyombo vya habari. Ikafikia zamu ya jina la Eddy kuitwa, Akanyanyuka na kujiweka vizuri, kwa mwendo wa kujiaminai akatembea hadi akafika mbele, alipo simaa raisi pamoja na majaji. Akakabidhiwa biblia kama misingi ya viapo vinavyo tumiwa kwenye kipindi hichi cha kuapishwa na kama ni dini ya uislam, wanatuma msaafu na kama huna dini basi unanyoosha mkono wako bila kushika chochote.
 
“Mimi Eddy Godwin, ninaapa kwamba nitaitumikia katiba ya nchi hii, kwa kuilinda na kuitunza. Ehee Mungu nisaidie”
Watu wakapiga makofi, hadi raisi mwenye akaonekana kupiga makofi kuashiria kumkubali kijana huyu mdogo aliye mkabidhi majukumu yaliyo washinda wazee walio dumu kwenye serikali kwa miaka mingi sana. Eddy akapeana mikono na muheshimiwa raisi pamoja na majaji walio kuwepo katika eneo la hapo mbele kisha akarudi kuketi kwenye kiti chake.
                                                                                               ***
Msunyo mkali ukasikika ukitokea kwenye kundi la watu walio jikusanya kwenye mgahaw huu maarufu ulipo katika jiji la Nairobi, hadi watu walio kuwemo ndani ya mgahawa huu wakageuza shingo zao kumtazama mtu huyo aliye achia msunyo mmoja mkali. 

Wengi wao hawakushangaa sana kuona sura ya mtu huyo anaye onekana ni wamakamo kiasi, wanaamini watu wakisha fikisha umri kama huo mara nyingi huwa na matatizo ya akili, na wanafanyaga mambo ambayo mara nyingi yanapaswa kuweza kufanywa na watoto wadogo. Kila mmoja akaendelea na shuhuli yiliyo mpeleka hapo, huku baadhi yao wakiyapeleka macho yao kwenye tv. Inayo onyesha majirani zao nchi ya Tanzania wakiwaapisha mawaziri wao.
 
“Eddy nilazima nikuue kwa mikono yangu mwenyewe, hata kama umepewa uwaziri ni lazima nikuue tuu”
Mzee Godwin alizungumza huku akiachia msunyo mwengine ulio wafanya watu wote kumgeukia na kumshangaa, baadhi yao wakaanza kuzungumza maneno ya chini chini, wakimuhusisha na imani za kishirikina.

SORRY MADAM(2)  (Destination of my enemies)

Mzee Godwin akanyanyuka na kuacha noti ya shilingi elfu moja ya Kikenya na kuiweka kwenye meza kwa ajili ya chakula alicho kipata, moja kwa moja akelekea kwenye hoteli aliyo fikizia. Akaingia chumbani kwake na kujirusha kitandani huku hasira kali ikiwa imemtawala sana. Akanyanyuka kitandani, akatoa simu yake mfukoni na kupiga namba aliyo iandika kwa jina la ‘My M’. Simu ikaita baada ya muda ikapokelewa upande wa pili.
 
“Upo wapi?”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti nzito, iliyo endelea kujazwa uzito kwa hasira kali iliyo tawala moyoni mwake.
“Jamani baby hata salamu?”
“Nasamu sio muhimu sana, nijibu swali langu”
“Bado nipo Somalia”
“Ninakuhitaji kesho mchana uwe umesha fika hapa Nairobi?”
“Jamani Godwin kuna nini, mbona hahe hahe hivi, unadhani nitamuagaje huyu mume wangu”
“Mery nimekuambia kesho ninakuhitaji hapa Nairobi ukifika nipigie nikuambie nipo wapi unifwate sawa”
 
“Sawa mpenzi wangu”
“Ole wako kesho ipite pasipo kuzileta hizo pua zako nitakufanya kile ambacho hujawahi kufanyiwa”
“Godwin hayo nayo yametokea wapi, si nimekuambia kwamba nitakuja”
“Fanya hivyo”
Mzee Godwin akakata simu na kuitupia kitandani, akaanza kuzunguka zunguka ndani ya chumba hichi, huku kila alilo kuwa akilifikiria kichwani mwake akaona halipangiki, akapiga simu kwa muhudumu aweze kuletewa mzinga wa pombe kali aina ya whisky inayo itwa ‘Brandy’yenye kiwango cha alcohol(kilevi) asilimia stini(60%). Muhudumu aliye pokea oda hiyo akafanya kama alivyo agizwa na kuupekeka mzinga mpya kabisa pamoja na glasi. Akamkabidhi mzee Godwin, aliye fungua mlango na kumzuia muhudumu huyuo kuingia ndani ya chumba chake. Akatoa noti mbili za shilingi elfu kumi za Kikenya na kumkabidhi muhudumu.
 
“Chenchi chukua”
Mzee Godwin akafunga mlango baaya ya muhudu huyo kupokea pesa hiyo aliyo pewa kwani ni mara mbili ya bei ya mzinga huo, hata mshahara wake si wa kiwango hicho. Akaondoka kwa haraka, kuhofia mzee Godwin kufungua mlango wa chumba chake akahairisha kwa yeye kuchukua chechi iliyo bakia.
Mzee Gowdwin akaanza kufakamia mafumba ya pombe hiyo, iliyo tengenezwa katika mfumo wa Spirit, ambayo ni kali sana pele unapo idumbukiza mdomoni mwako, hususani kwa mtu ambaye hajawahi kuitumia pombe hiyo.
 
***
    Baada ya sherehe kumalizika, Eddy akamfwata mama yake aliye kuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wapya serikalini.
“Jamani huyu ni kijana wangu, ninaamini kwamba mumesha mfahamu”
“Tumemfahamu muheshimiwa”
“Jamani ninawaomba mumuunge mkono na mumuonyeshe njia kama vile mulivyo nipa mimi ushirikiano”
“Sawa muheshimiwa, tutahakikisha kijana anayooka”
Eddy akaendelea kutambulishwa kwa viongozi walio kuwa wakifanya kazi na mama yake katika kipindi chote alipo kuwa madarakani kama waziri mkuu. Ikawa ni moja ya hatua ambayo Eddy hakuitegemea sana kwenye maisha yake, na wala hakuwazia kama ipo siku atakuja kuwa kiongozi serikali.
 
“Eddy mwanangu”
“Naam mama”
“Nafasi ni hii, nakuomba nakuomba mwangu. Ufanya kazi vizuri, usije ukanidhalilisha hapo baadaye.”
“Siwezi kufanya hivyo mama yangu”
“Mimi nakuombea kwa maana ninafasi ya kipekee uliyo pata kuwa waziri pasipo kupitia ubunge”
“Sawa mama, nitajitahidi ninafanya kazi vizuri pale nitakapo kuwa ninahitaji msaada wako mama nitakujulisha”
Eddy alizungumza na mama yake wakiwa wamesimama kwenye moja ya bustani, iliyopo eneo la ikulu
“Vipi lakini kija Junio hawajambo?”
“Hawajambo wanaendelea vizuri”
“Kesho, nitatuma dereva aje kumchukua. Alafu anaanza lini shule?”
 
“Nataka nimpeleke bording school”
“Kwa nini?”
“Akakae huko”
“Sitaki mtoto aende bording akiwa bado mdogo, subiri asome afike lasaba ndio umpeleke bording”
“Nimekuelewa mama”
“Sawa naona wezako wanajipanga kwa kupiga picha ya pamoja na raisi, Nenda na wewe ukajumuike nao”
“Powa mama”
“Weee hiyo lugha za powa, naomba uziache ukisikiwa na hao mapaparazi utaonekana muhuni”
Eddy akaondoka huku akicheka, akajumuika na mawaziri wezake katika kupiga picha hivyo ya pamoja wakiwa na riasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani bwana Praygod Makuya.
                                                                                           ***
    Vyombo vingi vya habvari asubuhi iliyo fwata, stori kubwa ikawa ni kwa huyu waziri wa Ulinzi bwana Eddy Godwin, wengi wao waliingiwa na mashaka wakidai kwamba bwana Eddy alisha fariki miezi kadhaa ya nyuma, ila wengine walidai ni miongoni mwa wanasiasa wapya kuwahi kujitokeza kwenye serikali ya Tanzania pasipo kujinadi kwa wananchi.
 
Kila aliye kuwa akiitazama picha ya Eddy kwenye gazeti hakukosa cha kuzungumza huku wengine wakidai kwamba hato wajibika kama wanavyo hitaji wao awajibike. Wengine wakidai kwamba bwana Eddy Godwin amependelewa kutokana mama yake alikuwa ni waziri mkuu.
“Yaani hii nchi, imejaa ukiritimba sana”
Mwanafunzi mmoja wa chuo cha Mlimani alizungumza huku akipitia macho yake kwenye gazeti la G NEWS
”Kwa nini?”
Mwenzake aliye kaa naye kwenye kochi moja lililo tengenezwa na saruji, kwa ajili ya kujisomea alimuuliza mwenzake.
“Huyu waziri wa ulinzi kumbe mama yake alikuwa ni huyu mama waziri mkuu aliye jiudhuru”
 
“Ahaaa!!”
“Wewe shangaa tu, utasoma hapo hadi makalio yaote sugu, ila kuna watu kiulaini wanajichukulia vyeo serikalini”
“Daaaaa yaani hii nchi mbona inapelekwa kizembe hivi, hivi kwa nchi za wezetu ni lazima mtu awe na vigezo vya kielimu ndio awe waziri tena waulinzi. Sasa huyu mimi sijui hata kama ana cheti cha form six”
Wote wakacheke huku wakiendelea kutazama picha kadhaa, zikimuonyesha Eddy akiwa na mawaziri wezake pamoja na muheshimiwa Raisi. Mijadala ya kumjadili Eddy Godwin, ilizidi kusambaa kila kona ya nchi ya Tanzania huku wengine wakijipa matyumaini ya kumpa muda waziri huyu, huku wengine wakiukosoa uamuzi wa raisi kumteua mtu asiye fikia hata robo ya sifa ya kuwa waziri tena wa ulinzi.
 
    ***
    Haikuwa siku ngumu kwa Waziri Eddy Godwin, jambo la kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi yake, akafunga mlango wa ofisini kwake na kubaki peke yake, taratibu akapiga magoti chini na kuanza kusali
“Ehee Mungu, ninatambua una makusudi na mimi ya kuniweka kwenye hii ofisi, yenye sifa ya kuwashinda wengi na kupelekea malalamiko ya wananchi kwamba wanateseka. Ninakuomba uniopngoze na kunilinda, hadi mwisho wa kazi hii. AMEN”
 
Eddy akasimama, na kufungua mlango wake, kumruhusu sekretari wake kuingia.
“Muheshimiwa nimekuja kama ulivyo nihitaji”
“Ohhhh ulisema jina nani vile?”
“Stella”
“Stella nani?”
“Stella Msulwa”
“Ahaaa sasa fanya hivi, ninakuomba uwatumie Fax, wakuu wote wa polisi nchi nzima. Kesho waambie nina kikao muhimu nao”
“Sawa muheshimiwa, je utahitaji kahawa?”
“Hapana nipo vizuri”
“Asante mkuu”
Stella akatoka ofisini mwa Eddy na kurudi katika sehemu yake ya uwajibikaji wa kazi. Eddy akaanza kukagua faili moja baada ya jengine, huku akipitia baadhi ya madai yanayo toka kwenye jeshi la polisi wakiomba kuweza kulipwa madeni yao yanayo endelea kulimbikizwa na serikali pasipo sababu ya msingi.
 
“Bilioni thelethini, mmmmmm…….!!”
Eddy alishangaa deni hilo wanalo daiwa serikali na jeshi la polisi. Akachukua mafaili mengine kutazama mambo mengine yanayo husiana na wizara yake. Simu yake ya mezani ikaita, akaichukua taratibu na kuiweka sikioni mwake.
“Bosi kuna wageni wawili wamefika hapa wanahitaji kuonana na wewe”
“Ni wanawake au wanaume?”
“Mmoja ni mwana mama na mwengine ni mwanaume”
“Wamesema wametoka wapi?”
“Mwanaume ni kwenye moja ya kanisa, na mwanamke kwenye taasisi ya kusaidia watoto yatima”
“Po….ahaa, sawa waruhusu”
Eddy akairudisha simu yake kwenye sehemu alipo itoa, sekunde kadhaa mlango wa ofisisini mwake ukafunguliwa na wakaingia wageni wake walio kuwa wakimuhitaji. Mwanaume akawa amebeba brufcase nyeusi na mwana mama akiwa amebeba pochi kubwa, ambalo ni wamama wengi wa mjini ndio mikoba yao ya kisasa.
“Karibuni mukae wazee wangu”
“Asante muheshimiwa”
 
“Kwanza shikamoni, pili niwasaidie nini?”
Eddy alizungumza huku akiwatazama kwa umakini, kwa mbali akiachinia tabasamu dogo ili kuufuta umakini wake juu ya uso wake, ili wageni wake wasigundue hilo.
“Mimi ninaitwa mchungaji Mandingo, nimetokea kwenye kanisa la G.W.C”
“Mimi ni Madam Glory, ni mmiliki wa kituo cha kulele yatima kule Arusha kinaitwa M.C.C”
“Ahaaa nashukuru kuwafahamu, sasa twende kwenye mada husika iliyo waleta humu ofisini”
“Muheshimiwa sisi tulikuja kukupa kapongezi kadogo tu, kwa maana ni vijana wachache sana ambao wanapata nafasi ndogo kama hii”
Madam Grory alizungumza kwa kujichekesha chekesha
“Kamaa alivyo tangulia kusema mwenzangu, tumeona tuje leo ofisini mwako tukupe japo vijisenti kidogo kama pongezi”
Mchungaji Mandingo, akafungua brufcase yake na kuiweka juu ya meza, akaifungua, macho ya Eddy yakatua kwenye vibunda vipatavyo kumi na tano vya shilingi elfu kumi kumi, kisha macho yake akayahamishia kwa mchungaji Mandingo na Madam Glory.
 
“Ni shilingi hizi?”
“Ahaa muheshimiwa hizo ni vijisenti tu, vichache tu”
“Hujanijibu swali langu, ni shilingi ngapi?”
“Milioni hamsini tu”
“Ahaaa, sawa nashukuru kwa hilo, ila ngona niende hapo nje ya ofisi yangu mara moja kuna kitu nikachukue”
“Sawa mheshimiwa”
Eddy akasimama kwenye kiti chake na kujiweka vizuri shati lake jeupe alilo livaa, akapiga hatua hadi mlangoni mwake, akashika kitasa na kuufungua mlango. Akapiga hatua hadi walipo askari wanao linda ofini mwake. Akawanong’oneza kisha akarudi ofisini mwake na kuwakuta mchungaji Mandingo na Madam Mery wakiwa wanajichekesha chekesha, huku brufcase ikiwa bado wazi na vibunda vyake vikiwa kama alivyo viacha.
 
”Samahani jamani kwa kuchelewa”
“Usijali mtoto wetu, ila kuna makubaliano kidogo tungeomba utusaidie muheshimiwa”
“Makubaliano gani?”
“Sisi japo tunadili na jamii, ila kuna vijibiasahara vidogo vidogo tunavifanya. Tungeomba ulinzi wako muheshimiwa”
“Ahaaa ni biashara gani wazee wangu, ina bidi tuwekane wazi hata siku likitokea la kutokea tunalindana”
Mchungaji Mandingo na Madam Grory wakatabasamu, huku wakitazamana. Eddy naye akafwatisha tabasamu lao, taratibu Madam Grory akajivuta mbele kidogo na kumsogelea Eddy 
 
“Madawa ya kulevya na viungo vya albino”
Madam Grolry akajirudisha taratibu huku akiwa na tabasamu lake lile lile alilo kuwa ameloweka hapo awali, Mchungaji Mandingo naye akalisindikiza tabasamu lake kwa kutingisha kichwa akishiria kwamba, msaada wao ndio huo. Eddy hakuonekana kustuka sana, alicho kifanya ni kujikooholesha kidogo kama mtu anaye hitaji kulisafisha koo lake ili aendelee na mazungumzo hayo ambayo ni nyeti sana kwa Madam Grory pamoja na Mchungaji Mandingo.
Kundi la askari wapatao wanne wakiwa na silaha zao mikononi, wakaingia ofisini mwa waziri Eddy, baada ya kusikia sauti ya kujikoholesha, ambayo Eddy aliwaashiria vijana wake kwamba atafanya hivyo, na wao wausubirie mguno huo nje ya mlango.
 
“Ahaaa wazee wangu, tutakuja kuzungumza vizuri mukiwa polisi au mahakamani, Sawa wazee wangu?”
Mchungaji Mandingo na Madam Grory wakabaki wakiwa wameshangaa, miili yao ikaanza kutetemeka, kila mmoja akaanza kupata fukuto la mwili, ambalo hajawahi kulipata tangu alivyo zaliwa, japo kuwa ndani ya ofisi hii, hewa safi ya kijiubaridi(AC), iliendelea kupenya kwenye kila mwili wa mtu aliyomo ndani ya ofisi hii, ila wao hawakuihisi kabisa juu ya ngozi zao.
“Mu…muhe…eees…himi…wa”
Mchungaji Mandingo alipata kigugumizi cha gafla, ila Eddy hakujali kubabaika kwake, alicho kifanya ni kuwaamrisha vijana wake kuweza kuwanyanyua na kuwapiga pingu wahalifu hao, huku brufcace yao, wakiwa wameibeba wao wenyewe.
 
“Niwakute kituoni, pamoja na udhibitisho wao huo”
“Sawa mkuu”
“Byeee”
Eddy akawaaga, huku akitabasamu. Waalifu wake wakatolewa nje ya ofisi yake, akabaki peke yake, akafungua vifungo viwili vya shati lake na kuilegeza tai yake, kisha taratibu akajiegemeza kwenye kiti chake.
‘Ahaa kumbe hawa ndio wanao waumiza walala hoi na kuwatesa walemavu wa ngozii’
Eddy alizungumza huku akiendelea kuzunguka zunguka kwenye kiti chake.
                                                                                        ***
    Mlio wa simu, ukamkurupusha Mzee Godwin, kutoka kwenye usingizi wake mzito, ulio sababishwa na msongamano mkubwa wa mawazo pamoja na pombe kali aliyo ifakamiaa jana usiku. Kwa macho yaliyo jaa usingizi, akalitazama jina lililo jitokeza kwenye simu yake, ila akaiona namba ngeni. Taratibu akaiipokea na kuiweka sikiono mwake.
 
“Haloo”
Alizungumza kwa sauti nzito aliyo jaa, usingizi mkubwa.
“Baby jamani mbona unanifanyia hivyo, napiga simu kwa namba yangu hupokei, hadi nimeazimisha namba ya mtu mwengine”
Sauti ya malalako ya Madam Mery ilisikikika upende wa pili wa simu.
“Nilikuwa nimelala”
“Sawa niambie upo hoteli gani?”
Mzee Godwin akamtajia Madam Mery, hoteli aliyopo. Madam Mery akaahidi kufika baada ya masaa kadhaa katika eneo hilo.
Baada ya dakika kadhaa kama alivyo kuwa ameahidi Madam Mery, akafika kwenye hoteli aliyo ambiwa na Mzee Godwin, moja kwa moja akaeelekea kwenye chumba cha mzee Godwin. Akagonga mara kadhaa na mlango ukafunguliwa na mzee Godwin.
“Karibu ndani”
“Asante”
Mzee Godwin akafunga mlango  kwa ndani, Madam Mery akapiga hatua hadi kwenye kitanda na kujitupa, hii ni kutokana na uchovu wa safari kutokea Somalia hadi Nairobi Kenya.
 
“Eheee mbona jana umenipigia simu ya hae hae vile?”
“Nina mazungumzo na wewe, hivi una habari gani kuhusiana na Eddy?”
“Kwakweli sina ni muda mrefu sijaonana naye, nahisi atakuwa amekufa”
Madam Mery alizungumza huku akihitaji kujua ni kitu gani kinacho endelea baina ya Godwin na Eddy
“Yule mshenzi amepewa uwaziri wa ulinzi Tanzania?”
“Mungu wangu………ana sifa gani za yeye kuwa waziri?”
“Ndio hivyo. Yaani laiti ningejua huyu mchenzi ningemuua tangu tukiwa ndani ya ndege ninaamini kwamba tusinge kuwa tunazungumza mazungumuzo ya kumuuhusu huyu kibwengo mtu”
“Kwa nini usimuue?”
“Mazingira hayakuruhusu, alipelekea kunipa shida ya kutafutwa hapo bendeni kwa hayati Mzee Madiba”
“Ulitokaje tokaje ndani ya ndege?”
Swali la Madam Mery likamfanya Mzee Godwin kurudisha kumbukumbu zake nyuma kwa haraka hadi siku aliyo toka kupambana na Eddy ndani ya ndege na taratibu akaanza kusimulia.
  
==> ITAENDELEA

No comments:

Powered by Blogger.