Trending News>>

USITAKE KUPITWA NA STORI KALI YA KUSISIMUA INAYOLETWA KWAKO NA MTUNZI MAHIRI..

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU: YA NANE
MTUNZI: Mr ManyamaJr
MAWASILIANO: 0767464766


ILIPOISHIA: 
"Hebu acha maneno yako wewe," alijibu Dokta Kisarawe huku akimalizia kufunga kufuli la mlango.

YUMBAYUMBA NAYO SASA

"Kha, dokta mbona sikuelewi?"
"Hunielewi kivipi wewe?"
"Si hivyo, ina maana kweli hujui kilichonileta?"
"Sasa kama ningekuwa sijui si ningekuuliza?"

Sulee alibaki kimya. Akawa hana cha kujibu wala kuongezea kwa hapo. Majibu ya mkato ya Dokta Kisarawe yalikuwa yamemuumiza na kumvunja moyo vibaya mno.

"Unajua Sulee mimi nakushangaa sana" Dokta Kisarawe alifungua tena uwanja wa mazungumzo baada ya Sulee kubaki kimya.

"Wewe unanishangaa mimi, au mimi ndiyo nakushangaa wewe?"

"Kwani, hebu ngoja nikuulize, hivi inawezekana kweli nikawa nawaita wagonjwa wengine, hadi nafunga mlango halafu nisijue kilichokuleta, inawezekana kweli?"

Sulee alibaki kimya tena, akawa anamwangalia Dokta Kisarawe kwa macho ya unataka kusema nini sasa?'

"Sikiliza, nina mazungumzo na wewe nje ya mazingira haya ya kazi, ndiyo maana sikutaka kukuita toka mwanzo," alisema Dokta Kisarawe na kumfanya Sulee aachie tabasamu kwa mbali.

"Hapo sawa, kwa hiyo tunaelekea wapi?"
"Wewe tulia, si uko na mimi sasa wasiwasi wako nini;?"
"Mmh!", Sulee aliishia kuguna.

Dokta Kisarawe akanyanyua simu na kupiga upande wa pili, ambapo ndani ya dakika kumi na tano, ilikuja teksi na kusimama karibu kabisa na walipokuwa.

Sulee akaelewa kuwa kumbe ile simu ilikuwa ni wito wa teksi. Kwa tahadhari kubwa sana, Dokta Kisarawe akampa ishara Sulee ya kumtaka akae siti ya nyuma.

Yeye akakaa mbele na dereva. Safari ikaanza huku Sulee asijue walipokuwa wakielekea.

Akataka kuuliza lakini dhamira ikamsuta na kubaki na maswali yasiyokuwa na majibu.

"Sijui tunaelekea wapi jamani?"
"Lakini namie bwana, si nimeambiwa nitulie kwa kuwa niko naye!"

"Lakini hata kama, sasa ndiyo napelekwa pelekwa tu kama mbuzi;” alizidi kuwaza lakini wakati akiendelea na mawazo hayo, ghafla mazungumzo yake na Dokta Kisarawe yakajirudia kichwani kwa kasi ya ajabu.

"Haa, sasa Dokta mbona unaondoka vipi kuhusu mimi jamani?"
"Kuhusu wewe nini tena"
"Si tiba yangu"
"Ipi?"
"Ya siku zote, ina maana umesahau kabisa?"
"Hebu acha maneno yako wewe"
"Kha, dokta mbona sikuelewi?" 

"Hunielewi kivipi wewe?"
"Si hivyo, ina maana kweli juhui kilichonileta?"
"Sasa kama ningekuwa sijui si ningekuuliza?"
"Sikiliza, nina mazungumzo na wewe nje ya mazingira haya ya kazi, ndiyo maaana sikutaka kukuita toka mwanzo.
"Hapo sawa, kwa hiyo tunaelekea wapi?"
"Wewe tulia, si uko na mimi sasa wasiwasi wako nini? Ikabidi atulie.
"ngoja nione mwisho wa safari hii"
 akawaza moyoni huku akiegemea kwa nyuma.

Safari ikaendelea, mbele kidogo dereva alianza kupunguza mwendo, Sulee alipochungulia kupitia kioo, akasoma bango lililoandikwa Utulivu Gest House.

Moyo ukamlipuka, akajua nikilichokuwa kinaendelea.

Baada ya kuteremka, dokta alimlipa dereva pesa yake na kumruhusu aondoke zake lakini akamwambia angempigia simu baaadaye kwa ajili ya kwenda kuwapokea. Alionekana kuwa ni mtu wake wa karibu sana, ndiyo maana Dokta Kisarawe alikuwa anamuamini kwa kiasi kikubwa namna hiyo.

Wakazama hadi mapokezi ambapo baada ya kukamilisha taratibu zote, wakapewa chumba.

Walipoingia tu, Dokta akaanzisha mazungumzo.

"Umeona mwisho wa safari yetu;?"

"Nimeona, umeshinda bwana"

"Ulikuwana wasiwasiii?"

"Mmh;" 

Dokta Kisarawe alimwambia Sulee kuwa alikuwa mjamzito jambo lililomshangaza sana Sulee.

"Unasema kweli dokta?"
"Wewe niamini mimi;"
"Kweli?"

"Ili uhakikishe, naomba kesho ukapime kwa daktari mwingine halafu uje uniambie."

Waliongea mengi lakini mwisho wa siku wakaelekea kwenye uwanja wa fundi seremala ambapo shughuli ilikuwa pevu, Sulee alijiachia na kutamka maneno yote aliyoyajua. Hatimaye walifika pamoja mwisho wa safari yao.

Baada ya shughuli hiyo, Sulee aliingia bafuni kujiweka sawa, na kisha kutoka ambapo alichukua usafiri hadi nyumbani kwake.

"Mbona leo umechelewa sana kurudi?" Mumewe Sulee, Masofa alimuuliza akiwa amekunja ndita.

Ilikuwa ni kama saa mbili na dakika kumi usiku kwa wakati huo.

"Watu walikuwa wengi sana, halafu nina habari njema sana mume wangu;"

"Habari gani hiyo?"
"Nina mimba"
"Amekupima;?"
"Sasa asingenipima ningejuaje?"
"Ok, mimi siamini labda twende kwa daktari mwingine"
"Sawa"

Waliongozana hadi kwenye zahanati ya jirani, na kumkuta daktari akiwa peke yake.

"Karibuni jamani"
"Ahsante;"

Walieleza shida zao, taratibu zikafanyika na baada ya dakika ishirini, waliitwa na daktari huyo.

********* 
JE SULEE NI MJAMZITO KWELI? AU DOKTA KAMDANGANYA?USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA.

No comments:

Powered by Blogger.