SIMBA YAREJEA KILELENI MWA LIGI KUU,YAITANDIKA NDANDA FC.
NaJuma Kaokote ,Mtwara
Timu ya Simba imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ndanda Fc mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili huku kosa kosa ziliendelea kutawala katika mchezo huo na dakika ya 38 Simba walipata pigo kwa kiungo wao mkabaji raia wa Ghana James Kotei kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Yassin Mzamiru hadi mapumziko Timu zote zilikwenda nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuingia kwa kusaka pointi tatu muhimu ili kupaa kileleni na katika dakika ya 63 Yassin Mzamiru aliwanyanyua mashabiki wa Simba waliofurika uwanjani baada ya kuingia goli hilo vijana wa Joseph Omog waliendelea kulisakama lango la Ndanda Fc.
Ibrahim Mohamed alipigilia goli la pili dakika ya 81 akiachia shuti kali lilojaa langoni na kumuacha mlinda mlango Jeremiah akiwa hana la kufanya hadi mwamuzi anamaliza Simba wameibuka na pointi tatu na magoli mawili na kuvunja mwiko wa Ndanda Fc wa kuzifunga timu kubwa kwenye uwanja wao kwani mzunguko wa kwanza waliweza kutoka sare na Yanga na kuwafunga Azam Fc 2-1.
Kwa matokeo hayo Simba wameishusha Yanga kileleni wakiwa na pointi 38 huku Yanga wakibaki kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 35.Matokeo mengine African Lyon wamewabana mbavu Azam Fc kwenye uwanja wa Uhuru na kugawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya 0-0.
No comments:
Post a Comment