Trending News>>

Hivi ndivyo Mchaparo wa Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania ulivyofana

Katika kuelekea mwisho wa mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2017, Kampuni ya EY Tanzania, imewakutanisha pamoja wafanyakazi wake katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.

Hafla hiyo, iliyoambatana na zoezi la utoaji wa tuzo kwa wafanyakazi bora wa mwaka 2016, ilinogeshwa pia na burudani ya muziki kutoka Bendi ya Malaika chini ya Mwanamuziki Christian Bella anaetamba na nyimbo zake kadhaa.
Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya EY Tanzania, Joseph Sheffu akizungumza katika hafya hiyo, ambapo aliwapongeza wafanyakazi wake hao kwa namna wanavyofanya kazi kwa bidii na kujituma, na kuwataka kuongeza bidii zaidi kwa mwaka ujao.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania, wakijiandaa kufungua shampein katika katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania, wakigonganisha glass ikiwa ni ishara ya kutakiana heri ya kufunga mwaka wa kazi katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
 
Mwanamuziki Christian Bella akitoa burudani kwa Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania, katika hafla ya kufunga mwaka iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.













No comments:

Powered by Blogger.