POLISI Agoma Kumtaja ‘Dikteta Uchwara’ Kizimbani
ASP Kimweli, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni shahidi wa pili katika kesi inayomkabili Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki, amepata kigugumizi cha kumtaja diktekta uchwara katika ushahidi wake, anaandika Faki Sosi.
Tundu Lissu anatuhumiwa kufanya uchochezi akisema “Dikteta uchwara” anapaswa kupingwa na watu wote.
Akitoa ushahidi wake leo, ASP Kimweli mbele ya Godfrey Mwambapa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu alieleza kuwa terehe 28 Juni mwaka huu katika viwanja vya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu alimsikia Lissu akitoa maneno ya uchochezi.
Akiongozwa na Mohammedi Salum wakili wa Serikali alidai kuwa alimshudia Lissu akitoa maneno ambayo yangeweza kuwashawishi wananchi waipinge serikali yao.
Baada ya ASP Kimweli kueleza hayo ,Peter Kibatala wakili wa upande wa utetezi alimuuliza Shahidi huyo kuwa Dikitekta uchwara ni nani? Ndipo aliposema hamjui.
Kibatala : Ni sahihi kuwa unayoyaongea Mahakamani, mliyajadili na wakili wa serikali hapo nje?
ASP Kimweli: Sio sahihi.
Kibatala: niliwasikia mkijadili kuhusu hii kesi hapo nje.
ASP Kimweli: Tumeongea mengi pamoja na masuala kesi.
Kibatala: Mpaka unaenda Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati ulijua kuwa hilo ni kosa. Je ni nani aliyetajwa kuwa ni dikteta uchwara?
ASP Kimweli: Simjui, lakini Lissu alisema kuwa hata kama amechaguliwa na wananchi.
Kibatala: Ni sahihi kuwa wapo wengi wanaochaguliwa na wananchi.
ASP Kimweli: Ndio.
Je, unajua kuwa hapa Tanzania askari wetu wanaenda kupambana vita nchi jirani kupinga utawala wa uonevu na udikteta?
ASP Kimweli: Ni kweli.
Kibatala: Ni sahihi kuwa Mwalimu Nyerere alipinga udikitekta?
ASP Kimweli: Ndio.
Kibatala: Katika maneno aliyoyasema Lissu alieleza ni nchi gani na dikteta apingwe kinamna gani?
ASP Kimweli: kimya.
Maswali magumu
Naye Jeremia Mutasebya wakili wa upande wa utetezi aliongeza maswali ambayo yalikuwa magumu kujibiwa kwa upande wa shahidi.
Mutasebya: Ni Kosa au sio kosa kwa mbunge wa upinzani kuwaalika wananchi wawapinge wanasiasa wengine kwa njia ya kupiga kura.
ASP Kimweli: sio kosa.
Mutasebya: Je kwa ufahamu wako chama cha Demokrasia na Maendeleo kipo kuhalali.
ASP Kimweli: ndio.
Mutasebya: Ni kosa au sio kosa kwa chama cha upinzani na kukiondoa kukipinga chama tawala madarakani.
ASP Kimweli: Sio kosa.
Mutasebya : Je ni sahihi kwa Mbunge wa upinzani kupinga kwa nguvu zote serikali iliyokuwepo madarakani kwa kutumia nia ya kidemokrasia.
ASP Kimweli: Kimya.
Mutasebya: Kwa ufahamu wako Tanzania ni nchi ya kidemokrasia au ya kidikteta?.
ASP Kimweli; Demokrasia.
Mutasebya: Je dikteta ni neno la kisiasa.
ASP Kimweli: Ndio.
Mutasebya: Je, siku ile kulikuwepo na waandishi wa habari na walitoa zile habari kwenye TV, redio na magazeti?
ASP: Ndio.
Mutasebya: Katika maelezo yako ulisema kuwa maneno yale yangeweza kusababisha wananchi kushawishika kuipinga serikali yao. Je tangu siku hiyo ulisikia tukio lolote linalotokana na maneno ya Lissu?
ASP Kimweli: Sijasikia.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 18 Januari mwakani kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

No comments:
Post a Comment