Picha: Zari na Diamond wapata mtoto wa pili
Hayawi hayawi na sasa yamekuwa. Hatimaye Zari The Bosslady na Diamond wamefanikiwa kumpata prince wa familia aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa.
Kwa mujibu wa picha zinazoonekana sehemu mbalimbali mitandaoni zinaonyesha kuna kila dalili kuwa Zari ameshajifungua kwenye hospitali ya Netcare Pretoria East Hospital iliyopo mjini Pretoria aliyokuwa amepelekwa wiki hii.
Ni ngumu kuthitisha hilo kwa sasa kwa kuwa hakuna hata mtu wa karibu wa familia hiyo aliyepost picha yoyote inayoonesha kinachoendelea lakini inaweza ikawa ni rahisi zaidi kutambua hilo. Naomba nikurudishe nyuma kidogo kuangalia picha za Zari alizopiga kabla hajapelekwa hospitalini, alikuwa na msuko unaofanana na unaomuonyesha akiwa hospitali.
Na hizi ni picha zitakazokupa ukweli wa hili:
Tunawapongeza Diamond na Zari kwa kujaaliwa kupata mtoto wa kiume.
No comments:
Post a Comment