Trending News>>

MKHITARYAN KUREJEA KRISMASI


Meneja wa Manchester  United Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Henrikh Mkhitaryan atakosa mchezo wa EPL leo usiku dhidi ya Crystal Palace, lakini ana matumaini kuwa mfungaji huyo wa bao la ushindi dhidi yaTottenham atarejea kikosini hivi karibuni.

Henrikh Mkhitaryan

“Natumai Mkhitaryan anaweza kucheza wakati wa Krismasi,” alisema Mourinho kwenye kikao na waandishi wa habari kabla ya mechi.

Mourinho ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwa sababu atakosa mechi katika kipindi cha ubora wake, lakini angalau hawatampoteza kwa muda mrefu.

henrikh-mkhitaryan

Hata hivyo kocha huyo wa United amepata fursa nzuri kwenye eneo la ulinzi baada ya Eric Bailly kupona huku Phil Jones na Marcos Rojo wakirejea kwenye kiwango kizuri.


No comments:

Powered by Blogger.