Trending News>>

GUARDIOLA-HAPA NI MWENDO WA ‘TIK TAK’ TU

Kuna watu hawajawahi kuamini katika kushindwa. Kama na wewe upo upande huo basi unaungana na Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ambaye pamoja na kujua kuwa endapo atashindwa kupata matokero mazuri anaweza kufukuzwa kazi lakini amesisitiza kuwa  hawezi kubadili mtindo wake wa kucheza.

pep guardiola

Manchester City ilianza msimu vizuri chini ya Pep Guardiola, ikishinda mechi zake 10 za mwanzo katika mashindano yote. Lakini kwasasa ipo katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya EPL ikiwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara Chelsea.

“Soka haipo kama miradi mingine inayochukua muda mrefu, unatakiwa kushinda mara zote na kama haushindi lazima uwe kwenye wakati mgumu”, Guardiola aliwaambia waandishi wa habari.

pep-guardiola

Pamoja na hayo lakini Guardiola aliweka wazi hana nia ya kuacha utamaduni wake wa kucheza mpira aina ya ‘TIK TAK’, bali ataendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyopo ili mwisho wa siku klabu ifanikiwe pamoja na mchezaji mmoja mmoja aweze kufanikiwa kuongeza kiwango.


No comments:

Powered by Blogger.