Mh.Magufuli azuia kuhamisha wamachinga Mwanza
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemwagiza waziri na katibu mkuu Tamisemi kusitisha mara moja zoezi la kuwahamisha wamachinga katika Jiji la Mwanza mpaka hapo mamlaka husika itakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amesema ameitwa leo, na kuambiwa na Rais kuwa miongoni mwa vitu vinavyomkera ni namna wamachinga hao wanavyohamishwa.
Amesema siyo kuwahamisha tu, bali wanavyohamishiwa katika maeneo ambayo ni ngumu kupata wateja .
"Natoa maagizo kwa wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji wa mamlaka za Serikali za Mitaa kusitisha mara moja shughuli hiyo hadi utakapoandaliwa utaratibu wa maeneo mazuri ya kufanyia biashara na kuwashirikisha wamachinga wenyewe," amesema Simbachawene.
Simbachawene amesema mbali na tamko hilo, maagizo ya maandishi yatafuata kwa wahusika wote.
No comments:
Post a Comment