Trending News>>

ENDELEA KUWA UPDATES KWA KUSOMA HADITHI ZA KUSISIMUA NA KUBURUDISHA

SIMULIZI: DOKTA SIUMWI HUKO
SEHEMU: YA KUMI
MTUNZI: Mr ManyamaJr
MAWASILIANO: 0767464766


ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Kwa kutumia tundu la komeo la mlangoni, Sulee alichungulia ndani.
“Duh! Yaani kweli…?” Sulee alitamka maneno hayo baada ya kuona kwa ndani.

BURUZANA NAYO SASA…

Akarudi na kukaa tena kwenye benchi kama zamani, lakini akawa hatulii sehemu moja…

Kila mara alikuwa akiinuka kukaa, mara asogee mbele na nyuma, hakika wivu ulikuwa ukimpeleka vibaya…

“Haiwezekani, huyu Dokta Kisarawe anaweza kutuchanganya na rafiki yangu kweli? Hapana haiwezekani…,” Sulee akawa anawaza moyoni.

Baada ya muda mfupi, kilisikika kimya kutoka chumbani kwa Dokta Kisarawe. Baadaye akatoka Monica lakini uso wake ulikuwa haueleweki.

Kwa mbali alionekana mchovu kwa shughuli fulani lakini pia wakati mwingine alionesha uso wa uchangamfu na kuzidi kumchanganya zaidi Sulee.

“Vipi…,” Sulee alimuuliza Monica wakati wakiongoza njia ya kurudi nyumbani.
“Safi tu…”
“Umeonana na dokta…?”

“Sijaonana naye…,” Monica alimjibu Sulee huku akimkazia macho.
“Hujamuona…!?,” Sulee akauliza kwa sauti ya mshangao mkubwa.

“Sulee bwana, sasa wewe unajua kabisa niliingia ndani kwa dokta tena wewe ndiye uliyenipeleka, sasa unaponiuliza kama nimemuona dokta ulitaka nikujibuje? Basi sijamuona…,” Monica alijibu huku akimtazama Sulee kwa jicho la ‘Uwe unafikiri kabla ya kuuliza swali’.

Sulee akakaa kimya na kumuangalia Monica kama anayesema ‘Leo umeniweza’.

Wakaendelea na safari yao, lakini Sulee hakuwa amejiridhisha na majibu ya Monica hivyo akaendelea kumdadisi zaidi kujua kilichoendelea kati yake na Dokta Kisarawe.

“Oke, kasemaje…?”

“Amenipima na kunipa dawa hizi, lakini ameniambia nirudi baada ya siku mbili…,” Monica alimjibu Sulee na kumuonesha dawa ambazo alikuwa amepewa na Dokta Kisarawe.

Moyoni Sulee alijisikia wivu zaidi kwani hata yeye mara ya kwanza kuonana na Dokta Kisarawe alipimwa na kisha kupewa dawa na kuambiwa arudi baada ya siku mbili.

Hisia za Dokta Kisarawe kufanya kama alivyomfanyia yeye zikazidi kumgubika moyoni.

“Siku ya kurudi utaniambia ili twende wote, sawa…?”
“Sawa…,” Monica alijibu kwa mkato na sauti ya chini mno.
“Mbona kama umeishiwa na raha Monica…?”

“Hamna, mbona niko kawaida tu Sulee…”
“Au umeambiwa nini na Dokta Kisarawe…?”
“Hakuna kitu Sulee, niko sawa…”

Waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale, lakini Monica alionesha wazi kuwa hakuwa sawa kabisa, jambo ambalo lilizidi kumuweka njia panda Sulee.

Baadaye waliagana na kila mmoja kwenda nyumbani kwake kwani tayari ilishakuwa usiku wa saa tatu kama na robo hivi…

Monica akiwa njiani, alianza kuwaza mambo mengi sana, lakini kubwa ni kwa nini Sulee aendelee kung’ang’ania kwenda naye mara ya pili wakati alishamuelekeza.

“Aah wapi, naenda peke yangu, si ameshanionesha…?” Monica akaendelea kuwaza na kufikia uamuzi wa kutokwenda na Sulee mara ya pili.

**************
Baada ya siku mbili, Monica aliamua kwenda kwa Dokta Sulee peke yake bila kumtaarifu Sulee…

Baada ya kutimu saa moja na nusu karibia saa mbili, Sulee akazidi kushangaa kwa nini Monica hakumpitia kama walivyokubaliana.

“Huyu mbona hajafika hadi sasa hivi, au kaghairi…?” Sulee alizidi kuwaza baada ya kuona muda unazidi kusonga mbele bila kumuona rafiki yake Monica.

Akachukua simu na kujaribu kumpigia ili amuulize kama alikuwa ameghairi kwenda kwa dokta.

Simu ya Monica iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya Sulee kurudia tena zaidi ya mara tano. Akazidi kuchanganyikiwa.

Akampigia Dokta Kisarawe, naye akawa hapokei. Akaamua kumpigia mume wake na Monica ili kujiridhisha. Mume wake Monica alimwambia Sulee kuwa rafiki yake huyo alikuwa ameenda kwa dokta.

Sulee akatulia. Baada ya kupita saa nzima, simu ya Sulee iliita na alipoitazama, alikuwa ni mumewe Monica akimtaarifu kuwa Monica amepokea na kumueleza kuwa anajiandaa kurudi. Sulee hakujibu kitu zaidi ya kulala.

Kesho yake, aliamua kwenda kimyakimya nyumbani kwa Monica. Baada ya kuzungumza, walikubaliana kwenda pamoja siku hiyo huku Sulee akimlaumu kwa kumuacha jana yake.

“Nilichelewa nikaona nitakusumbua shoga yangu,” alijibu Monica lakini akikimbiza macho yake chini kwa aibu f’lani hivi.

Ilipotimu jioni, waliongozana pamoja hadi kwa Dokta Kisarawe, walikuta wagonjwa wengine wamepanga foleni.

Mlango ukafunguliwa na Dokta Kisarawe akatoka, alipowaona haraka akamuita Monica na kuwaacha wagonjwa wengine, akafunga mlango. Sulee kuona vile, akasogea hadi mlangoni na kuanza kuchungulia tena.

Kwa mbali akaanza kusikia tena vitu vikisogezwa. Mara kikatokea kimya cha ajabu.

Baadaye kidogo, Sulee alisikia sauti ya kulalamika ya Monica akisema

Dokta mimi siumwi huko jamaniiii, mmh!.

ITAENDELEA…..

No comments:

Powered by Blogger.