Wakuu wa taasisi za umma waandaliwa kitanzi
Dodoma. Serikali imewasilisha bungeni muswada unaokwenda kuwatia kitanzi wakuu wa taasisi za umma watakaoshindwa kulipa mikopo iliyoidhamini na kuhakikisha inawekezwa kwenye miradi itakayosaidia kuilipa.
Marekebisho hayo ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana yamo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 4 wa Mwaka 2016 yaliyowasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni kwenye mkutano uliopita.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alisema marekebisho hayo yanapendekeza kuongezwa kwa vifungu vya sheria ambavyo vinaweka sharti kwa wizara na taasisi za Serikali ambazo zinaruhusiwa kwa mujibu wa sheria nyingine kukopa, kupata idhini ya waziri wa fedha.

No comments:
Post a Comment