RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 39 & 40
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Bwana Rusev aliendelea kutoa maelezo ya Hotel atakayo fikizia bwana Paul Henry Jr, akaonyesha kila sehemu ambayo bwana Paul Hery Jr atapita akiwa na watu wake wanao mlinda. Hadi mwisho wa maelekezo yake, wote wakawa wamemuelewa vizuri bwana Rusev.
“Agnes hii ni kazi yako ya kwanza na sinto hitaji ukosee, ninakuamini sana”
“Usijali mkuu nipo kwa ajili yako”
“NITAHITAJI UMUUE KIONGOZI HUYU IWE TISHIO KWA NCHI HII NA DUNIA NZIMA”
“SAWA MKUU”
Agnes alijibu huku akiinamisha kichwa chake chini kama ishara ya kumuheshimu bwana Rusev, kisha bwana Rusev akachuku moja ya chini yenye alama ya X na kumvisha Agnes shingoni, akampa Baraka kwa ajili ya kuitekeleza kazi hiyo hatari sana kwa maisha yake.
ENDELEA
Agnes akaanza kazi moja ya kulenga shabaha kwa masafa ya mbali pasipo kutumia lensi inayo saidia kuweza kuvuta vitu karibu, kila anacho kilenga kwa kutumia bunduki yake aina ya AS50 Sniper rifle, yenye uzito wa kila zaidi ya kumi na tano ikiwa na risasi zilizo jaa, akahakikisha anakipata vizuri huku akiwa ameishika mkononi mwake, jambo ambalo lilizidi kuwashangaza wengi kwani, hii ni bunduki ambayo mara nyingi mtu huwa anaiweka chini na kuisimamisha kupitia vimiguu viwili vya chuma, ili kuweza kulenga shaba.
“Waooooo”
Fetty alimpigia makofi Agens, baada ya kumkuta akiwa analenga vitu vya mbali kwa bunduki hiyo. Agnes baada ya kumuona Fetty akaacha zoezi lake ambalo analo kifanya
“Mwanangu kweli unatisha, hii ngoma ni nzito”
Fetty alizungumza huku akiinyanyua bundiki aliyo ishika Agnes
“Inahitaji mazoea kuweza kuitumia la sivyo unaweza ukafa, kwa maana ninapiga hadi nasikia mapigo ya moyo yanacheza kama kitenesi”
“Hahahaa, sas mtu wangu si uiweke chini ndio upige?”
“Ahaaa chini najiona kama nakosa shabaha vile”
“Ok tuachanane na hayo, vipi maandalizi yako ya kwenda kwenye hiyo mission?”
“Ndio kama hivi unavyo niona nazidi kujikaza, kwa maana nikicheza vibaya nakufa au nakamatwa na nisinge penda kukamatwa na wamarekani, ni bora nijipige risasi nife hapo hapo”
Maneno ya Agens yakamfanya Fetty kukaa kimya huku akimtazama Agnes usoni mwake, jinsi anavyo mwagikwa na jasho jingi.
***
Kila mmoja ndani ya maabara akaka kimya huku akimtazama Rahab, jinsi anavyo mchunguza mtu mmoja baada ya mwengine. Rahab akaachia tabasamu pana kisha akapiga hatua na kuingia ndani kabisa ya maabara huku nyuma yake akiingia mume wake pamoja na bosi wa bwana Frednando
“Jamani asanteni kwa ushirikiano wenu kwa kuweza kunihudumi hadi nimekuwa sawa”
Rahab alizungumza kwa furaha kubwa, ikamlazimu Frednando kuweza kuitafsiri kwa kispain. Madaktari walitabasamu kwa uwoga ila mioyoni mwao kila mmoja alikuwa akiliwazia lake kuhusiana na mbwa aliye fufuka dakika chache zilizo pita. Rahabu pasipo kuambiwa na mtu yoyote akaingia kwenye chumba alicho fungiwa mbwa huyo na kumchuku.
“Jamani mbwa huyu nimependa, anaitwa nani?”
Rahab akawauliza madaktari walio baki na mshangao mkubwa, kwa kingeraza ila mmoja wao akajikaza na kuzungumza kwa sauti ya utaraitibu.
“Anaitwa Charity”
“Waoo nitamchukua nimempenda sana”
Hakuana aliye kuwa na ubishi kuhusiana na kuchukuliwa kwa mbwa huyo, waliye mfanyia majaribio, ila kila daktari akabaki kimya. Hapakuwa na daktari aliye weza kuzungumza kwa kile walicho weza kukiona.
Wakarudi katika jumba la Frednando ambapo ikawalazimu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Mexco. Balozi baada ya kupokea simu ya raisi Praygod Makuya, ikamlazimu kuongozana na baadhi ya askari wa jeshi la Tanzania hadi kwenye jumba la Frednando, baada ya kufika wakapokelewa vizuri kama ilivyo kuwa kwa raisi wao.
“Yaani raisi siamini kama upo hai?”
Bi Joyce Maagi alizungumza huku akimtazama raisi Praygod machoni mwake.
“Nipo hai, nasikia nchini watu wapo kwenye maombolezo ya kifo change?”
“Ndio muheshimiwa hapa mwenyewe nilikuwa nimebakisha siku mbili niende kwenye msiba wako”
“ Ok ila sinto hitaji muweze kuzungumza kitu chochote kuhusiana na kuniona kwangu, nitahitaji kurudi siku ya mazishi yangu ninaamini nitakuwa Tanzania”
“Ila kikubwa ninacho hitaji wewe kukifanya nitengenezee mazingira katika uwanja wa ndege kwani nitakuja na private airplane(Ndege binafsi), wajulishe baadhi ya watu watakao nipokea kisiri mimi na mke wangu pasipo watu wengine kuweza kutambua lolote”
“Sawa muheshimiwa ila kuna swala la mke, si tayari amesha fariki au kuna mwengine”
“Yupo”
Raisi Praygod akamngong’oneza mmoja wa wahudumu Frednando na kumuagiza akamuite Rahab, naye akafanya hivyo. Baada ya muda Rahab akafika sebleni, akiwa amevalia gauni jeupe na refu lililo mpendeza sana. Bi Joyce Maagi akusita kumshangaa Rahab, kwani picha yake ipo kwenye moja ya watu wali angamia na ndege ya raisi.
“Huyu binti naye pia amepona?”
“Ndio amepona, ni mmoja wa watu walio weza kuyapigania maisha yangu hadi hapa nilipo”
“Ahaa”
Bi Joyce Maagi akanyanyuka na kwenda kusalimiana na mke wa rais, kwa heshima zote. Wakaendelea na mazungumzo ya kawaida. Siku iliyo fwatia Bi Joyce Maagi akaondoka akiwa na masafara wake kuelekea nchini Tanzania, kitu cha kwanza baada ya kutua katika uwanja wa mwalimu Jk Nyerere, akafanya maagizo yote aliyo agizwa na Raisi Praygod Makuya, japo baadhi ya watu walishangaa kusikia kwamba Raisi Praygod yu hai.
Maandalizi ya safari ya kurudi Tanzania, yakawekwa tayari na Frednando, akahakikisha kwamba kila kitu kipo salama na hakuna jambo baya ambalo litamdhuru raisi Praygod Makuya pamoja na mke wake. Ikawa ni siku nyingine ya huzuni kwa marafiki wawili Praygod na Frednando, kila mmoja Alisha mzoea mwenzake kwa kipindi kifupi walicho ishi, ila hapakuwa na jinsi yoyote yakufanya. Iliwalazimu kuweza kutengana tena na kila mmoja aweze kuendelea na majukumu yake anyo yafahamu.
“Shem siku une ikuli Tanzania”
Rahab alizungumza kwa furaha baada ya kuwaona Praygod na Frednando wakiwa wanalengwa lengwa na machozi ya uchungu
“Usijali Shem, nitakuja siku naamini nikija mutakuwa mumepata kijana mdogo”
“Hahaaa Mungu ni mwema, ombeni Mungu niwazalie kijana wa kiume ili aja kuwa raisi kama baba yake”
“Kwa nini usituzalie wa kike ili awe raisi labda wa kwanza, mwanamke kwa miaka hiyo ijayo?”
“Sawa Mungu ni mwema anaweza kutuwezesha katika hilo”
“Haya jamani niwatakie safari nje, ndege imesha washwa, hiyo mutaitumia katika matumizi yenu binafsi”
“Asante sana Frednando ndugu yangu”
“Na hao marubani kama nilivyo kuambia, nitawalipa mimi”
“Sawa kaka”
Raisi Praygod na Rahab wakaingia kwenye ndege, taratibu ndege hiyo yakifahari ikanza kuiacha ardhi ya Mexco na ndani ya dakika kadhaa ikawa angani. Raisi Praygod kila alipo mtazama mke wake, hakusita kuachia tabasamu pana usoni mwake, kwani uzuri wa mke wake mara nyingi ulimpa kujiamini na kujiona ni mwanaume kwenye bahati kwa kuweza kumpata msichana mzuri kama Rahab.
***
Ukimya mkubwa, umetawala kwenye kiwanja cha mpira, jijini Dar es Salaa, viongozi wote wa nchini Tanzania na wengine wakitoke nchi jirani pamoja na wananchi wengi wakiwa katika kuyaaga mabaki ya miilii ya waanga walio fariki katika ajali ya ndege ya Air foce, huku wakiamini kwamba kati ya miili hiyo iliyo ungua vibaya hadi haitazamiki, mwili wa Raisi Praygod Makuya utakuwepo miongoni mwa hiyo. Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali nao hawakuwa nyuma katika kusali sala ya mwisho ya miili hiyo.
Vilio vya wamama hadi wanaume walio shindwa kuzuia vilio vyao, viliendelea kusikika katika sehemu mbalimbali za uwanja. Wanajeshi wa kulinda usalama pamoja na jeshi la polisi nao waliweza kukusanyika katika eneo la viwanja huku kila mmoja akiwa katika kuangalia usalama wa viongozi katika eneo hilo unaenenda vipi.
Majira ya saa sita machana ndege ya raisi Praygod Makuya ikatua kwenye uwanja wa mwalimu Julius K. Nyerere, kwa usiri mkubwa alio weza kuutengeneza balozi bi Joyce Maagi, aliweza kumpokea Raisi Praygod Makuya, na moja kwa moja akampeleka nyumbani kwa waziri Mkuu, Bi Magret.
Wakapolekewa nyumbani kwa waziri mkuu ambae alisha arifiwa kuhusiana na ugeni huo, na kipindi ambacho watu wapo viwanjani aliweza kuigiza kupoteza fahamu, ambapo aliweza kukimbizwa hospitalini, akiwa njiani akazinduka na kumuomba dereva ampeleke nyumbani kwake ili akajipumzishe na hakuona sababu ya yeye kwenda hospitalini.
Alipo fikishwa nyumbani kwake akamuru madaktari walio mleta waweze kuondoka, huku moyoni mwake akiwa na siri kubwa ya ujio wa raisi Praygod Makuya.
Ndani ya muda mchache, gari mbili nyeusi aina ya arstorn martin, zikaingia kwenye geti la jumba lake lakifahari. Akiwa pamoja na wafanya kazi wake wa ndani pamoja na mke wake wakasimama sehemu gari hizo zitasimama. Raisi Praygod akashuka ndani ya gari akiwa na mke wake Rahab. Bi Magret hakuamini ujio wa raisi huyo ambaye anamchukulia kama mwanaye kutokana na upendo alio weza kumfanyia na kumpa cheo cha uwaziri mkuu.
Wakakaribishwa ndani, huku Bi Magreti akionekana kuwa na furaha kubwa sana, wakapata chakula cha mchana huku wakitazama jinsi mambo yanavyo endelea kwenye uwanja taifa wa mpira.
“Aloo kumbe watu wananipenda sana ehee”
“Sana tuu muheshimiwa, yaani mimi nilipo pokea kuhusiana na swala la msiba wako nilijisikia vibaya sana”
“Aisee pole sana mama yangu, huyu ni mke wangu anaitwa Rahab”
“Ahaa karibu sana mke mpya wa raisi”
Bi Magreti alizungumza kwa furaha na kuwafanya watu wote waliopo sebleni kucheka. Rahab katika kuzungusha zungusha macho yake sebleni akaiona picha kubwa ukutani ya kijana aliye ustua moyo wake.
“Yule ni nanii ukutani kwenye ile picha?”
Rahab aliuliza huku akiinyooshea kidole picha hiyo
“Yule ni mtoto wangu anaitwa EDDY GODWIN, na yule binti pale ni Mke wake mtarajiwa anaitwa SHEILA”
Bi Magret alizungumza kwa furaha, huku akichia tabasamu pana usoni mwake, jambo lililo uchoma moyo wa Rahab pasipo mtu yoyote kuweza kugundua hilo
SHE IS MY WIFE(40)
“Ila kwa sasa kijana huyo hayupo ndani ya nchi hii”
Bi Magret alizungumza huku kidogo tabasamu lake likipungua usoni mwake, Rahab akataka kuuliza kitu ila akanyamaza na kumtazama mume wake.
“Ok jamani tunafanyaje kwa maana ninahitaji kwenda kuzungumza na wananchi wangu niwezee kuwapa ukweli kuhusiana na kilicho tokea”
“Itabidi tuwasiliane na makamu wa raisi”
“Hapana sihitaji uwasiliane naye”
“Kwa nini muheshimiwa nisiwasiliane naye?”
“Kuna sababu nyingi tu zinazo pelekea usiwasiliane naye ila utakuja kuzifahamu baadaya usijali kwa hilo, ila ninacho hitaji ni kwenda kwenye uwanja wa taifa”
“Muheshimiwa huoni kama itakuwa ni harari sana kwa maisha ya wananchi walio kuwepo katika eneo lile wengine wanaweza kuona kama ni mzimu umefufuka kutoka kuzimu”
Balozi Joyce Maagi alitoa wazo
“Hapana, nahitaji kuingia uwanjani kisiri pasipo mtu yoyote kuweza kugundua, na nitahitaji kuweza kufika katika eneo walio kaa viongozi wa juu au nifike ile sehemu ambayo kuna kipaza sauti”
Kila mmojaa akaka kimya akimtazama Raisi Praygod alicho weza kukiamua.
“Basi inabidi ubadilishe mavazi muheshimiwa, ili usiweze kugundulika”
“Sawa nitafutieni kofia pamoja na tisheti hii hizi walizo vaa waombolezaji”
Raisi Praygod akaletewa ngua ambazo ziliweza kumbadilisha muonekano wake na kuwa kama mtu wa kawaidia sana. Hakutaka kwenda na Rahab, alicho kifanya akaomba kuongozana na dereva wa waziri mkuu ila watumie gari moja kati ya magari mengi yanayo tumika hapo nyumbani kwa waziri mkuu.
“Mutaniona kwenye kideo nyinyi subirini”
Maneno ya Raisi Praygod Makuya yakamchekesha kila mmoja aliye weza kuwa katika eneo hilo, akaingia ndani ya gari na kuondoka, njia nzima Raisi Praygod akawa anapangilia ni maneno gani ambayo atakwenda kuyazungumza mbele ya wananchi wake. Kutokana ni siku ya majonzi, yaliyo tawala nchi nzima, ndani ya jiji la Dar es Salaam, foleni haikuwa kubwa, askari wa ulinzi barabarani wametanda kila mahali wakihakikisha kwamba hakuna ujinga wowote ambao utajitokeza katika siku nzima ya leo.
Wakafanikiwa kufika katika uwanja wa taifa wa mpira, akamuamuru dereva kusimamisha gari kwenye maegesho ya watu wa kawaidia, kisha akashuka kwenye gari, akatazama kila pande, alipo weza kuona hakuna anaye mfwatilia zaidi ya askari wakiendelea kuzunguka zunguka wakiwa na mbwa wanao nusa harufu. Akaanza kupiga hatua za kawaidia kuelekea kwenye geti la kuingilia kiwanjani ambalo ni geti lililo pita magari ya waheshimiwa, na askari wengi waliweza kulinda geti hilo kwani hapakuwa na mtu aliye weza kuruhusiwa kuingia katika geti hilo. Akafika getina na mwanajeshi mmoja akamzuia
“Sahamani hakuna anaye ruhusiwa kupita katika geti hili, zunguka upande ule ndipo kwenye mageti yakuingilia wananchi wa kawaidia”
Mwanajeshi huyo alizungumza kwa lugha ya utaratibu huku kwenye mkono wake wa kushoto akiwa amejifunga kitambaa cheusi akishiria kwamba anaadhimisha msiba.
“Mimi nataka kupita hapa hapa”
“Samahani ndugu, nisinge penda kuweza kutumia nguvu kubwa ya kukutoa hapa. Tafadhali fwata maelekezo niliyo kuagiza uweze kufwata”
Raisi Praygod akatabasamu kisha akaipandisha kofia yake juu taratibu, jambo lililo mstua mwanajeshi huyo.
“Shiiii….usistuke mimi nipo hai, ila nahitaji msaada wako wakuingia humu ndani kupitia geti hili kwani itakuwa raisi kwa mimi kuweza kufika kwenye kipaza sauti. Ila tafadhali usimuambie mtu yoyote kama umeniona sawa”
Mwajeshi huyo akataka kupiga saluti lia Raisi Praygod akamkataza asifanye hivyo, akamsisitizia nia yake ni kuweza kufika kwenye kipaza sauti.
“Muheshimiwa mimi hapa cheo change ni kidogo, kama unavyo nioana wewe mwenyewe. Sina mamlaka ya kukupitisha pele labda nimuite mkuu wangu aje”
“Mimi nimekuomba wewe na si wale wengine fanya uwezalo niingie uwanjani. Kwanza jina lako unaitwa nani?”
“Thomas Makengele”
“Sawa bwana Makengele, fanya kazi niliyo kuagiza kuifanya”
“Sawa nisubiri dakika moja”
Thomas akakimbia hadi kwenye kibanda cha dharula kilicho yengenezwa pembeni ya geti akamuomba mkuu wake na kumuongopea kwamba kuna ndugu yake anahitaji kuingia ndani ya uwanja kwani mageti mengine watu wamejaa
“Sasa unataka kumruhusu akakae wapi, wakati geti hili ni kwaajili ya VIP tu”
“Nakuomba tu mkuu, atasimama hata pembeni ili kuweza kushuhudia kinacho endelea”
“Usije ukawa unatuuingizia jambazi, badae tuje kulamiana?”
“Hapana mkuu, nilikula kiapo kuitete, kuilinda nchi yangu na katiba yake. Siwezi kufanya ujinga kama huo”
“Mruhusu, tena hakikisha unamsindikiza hadi atakapo kaa, kwa maana na ushamba shamba wake anaweza kwenda sehemu ambayo mtu kama yeye haruhusiwi kwenda”
“Sawa mkuu asante sana”
Thomas akatoka akiwa na furaha kubwa moyoni mwake, kwani uongo wake umeweza kukubalika. Akamfwata raisi Praygod sehemu alipo simama.
“Muheshimiwa twende nikupeleke ndani”
“Sawa”
Kutokana na amri ya mkuu wa geti hilo, Thomas akafanikiwa kuingia ndani ya uwanja akiwa na Raisi Praygod ambaye hadi sasa hivi hajajulikana kama ni yeye
***
Jiji zima la Mossco nchini Rusia, limezungukwa na wanajeshi wa Marekani wakisaiidiana na wanajeshi pamoja na polisi wa nchini Rusia, kuendeleza kulinda usalama jiji zima, kwani ni masaa machache yamesalia kiongozi mkubwa dunia waziri wa mambo ya nje nchini Marekani bwana Pual Henry Jr. Kuingia katika jiji hili, kwa madhumuni ya kikako kikubwa ambacho ni moja ya kauli mbiu ya Marekani, kuyazuia baadhi ya mataifa yanayo jaribu kutengeneza silaha za nyukilia, kuachana mara moja na mpango huo, kwani ni harati kwa dunia nzima, endapo silaha hizo zitaweza kutumiwa.
Kila mwananchi aliweza kukaguliwa kwa vifaa maalumu, na askari ambao kila wakati hawakuhitaji kuona kuna jambo baya linaweza kutoke kwa kiongozi huyo mkubwa.
Agnes akiwa katika hali ya umakini mkubwa, akafanikiwa kuingia kwenye jiji la Mosscow, pasipo kuweza kukutana na kuzuizi cha aina yoyote. Kitu cha kwanza kuweza kukifanya, akaanza kutafuta ni wapi kwenye gorofa refu linalo karibiana na Hotel atakayo fikikizia bwana Paul Henry Jr. Akafanikiwa kuona moja ya gorofa lenye urefu wa gorofa zipatazo stini. Kwa kulichunguza kwa haraka haraka akagundua ni moja ya gorofa lenye ofisi nyingi za watu binafsi.
“Nitafanyaje?”
Agnes alizungumza huku akiwa amesimama nje ya jengo hilo, lenye watu wengi wanao ingia na kutoka. Kabegi kadogo alicho kavaa mgongoni, haikuwa ni rahisi kwa mtu kumstukia kwamba amebeba bunduki yenye uwezo mkubwa sana, kwani aliweza kuigawanya gawanya na kuwa ndogo sana inayo weza kubebeka ndani ya kibegi hicho kidogo.
Akaingia ndani ya jengo hilo, akaingia kwenye moja ya lifti na kiminya batani iliyo andikwa namba stini. Lifti hiyo ikaanza kwenda juu kwa kasi, hadi ikafika katika gorofa namba stini, mlango ukafunguka, kabla hajatoka akachunguza kordo nzima, akamuona dada mmoja akiwa anafanya usafi kwenye kordo hiyo, huku akiwa amevalia mavazi yanayo muonyesha ni muhudumu katika eneo hilo. Akatoka na kuanza kuelekea alipo dada huyo, huku akizitazama kamera za ulinzi zilizo tegwa kwenye eneo hilo.
“Samahani”
Agenes alizungumza kwa kingereza na kumfanya dada huyo kuacha alicho kuwa anakifanya na kumtazama
“Unajua kuzungumza kingereza?”
“Ndio zungumza tu”
“Nahitaji kwenda chooni, tafadhali naomba unisaidie”
“Ohooo, ofisi zimesha fungwa dada yangu, na kila ofisi ina choo cheke labda nikusaidie kwenye moja ya ofisi ambayo ndio ninakwenda kuifanyia usafi”
“Sawa nitashukuru”
Dada huyo akabeba vifaa vyake vya usafi, wakaongozana na Agnes hadi kwenye moja ya ofisi, wakaingia ndani.
“Kuna choo kile pale waweza kujisaidia”
“Ila kwa nini watu wamefunga ofisi mapema hivi?”
“Leo ni siku ya kuja kwa kiongozi mkubwa, basi watu tunakwenda kumpokea ndio mana ofisi nyingi zimefungwa mapema hii”
“Ahaaa sawa”
Agnes akaingia ndani ya choo alicho elekezwa, akavua koti lake dogo alilo livaa kutokana na baridi kali, kisha akavua na gloves nyeusi alizo zivaa. Akaminya kitufe kwenye choo cha kukalia na kuyafanya maji kuweza kuzunguka, ili kumdanganya dada huyo kwamba amemaliza haja yake ya kujisaidia.
Kabla hajatoka akasikia mlango ukigongwa, jambo lililo mfanya kujiandaa na kujiweka tayari kwa lolote kisha akamruhusu mtu anaye gonga kuweza kuingia ndani. Akaingia dada mfanyakazi huku akiwa na vifaa vyake, gafla Agnes akampiga ngumi nzito shingoni dada huyo na kumfanya aanguke mzima mzima kama mzoga.
No comments:
Post a Comment