Trending News>>

PPF MWANZA YAVUNA WASANII 202 WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.

Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akizungumza na baadhi ya wasanii  wa mikoa ya kanda ya ziwa mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mwishoni mwa wiki.

WASANI  202 wa mikoa ya kanda ya ziwa wajiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa Wote Scheme jijini Mwanza wakati wa warsha fupi ya kuwajengea uwezo wa sanii  iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa  jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi za uanachama wasanii hao Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe amesema wasanii mbali mbali wamejiunga katika mfumo ‘Wote Scheme’moja kwa moja   katika  Mfuko huo ambapo watapata mafao yanayotolewa na PPF 
moja kwa moja katika mfumo wa Wote Scheme ambapo mtaweza kupata huduma ya matibabu baada ya kuchangia miezi 3, 
 faida ni kupata mikopo ya biashara,  pamoja na mafao ya uzeeni.

Amewaasa wananchi wote wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawapo katika sekta rasmi kama madereva wa Tax, wajasiliamali, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na madereva wa bodaboda wajiunge na mfuko wa PPF ili waweze kunufaika na mafao mbali mbali.

Wasanii hao ni kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na  Geita, pamoja na kupata elimu kutoka PPF vilevile washiriki walipata fursa ya kujengewa  uwezo wa kuhariri kutengeneza Miswada ya filamu pamoja na umuhimu wa kujiunga na mifuko ya uchangiaji wa hiari kwa ajili ya manufaa yao wenyewe pamoja na familia zao.  

Kwa upande wa wasanii wamefurahia sana mfumo wa Wote scheme kwani umekuja wakati sahihi ambapo Mfumo huu wa PPF utawasadia kwa kuwezesha kupata mikopo ya maendeleo na Bima ya afya, hivyo kuwafanya kuendelea na maisha yao.
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa Mfuko wa PPF, Msanii wa Filamu jijini Mwanza, Mwanaharusi Hela ambapo zaidi ya wasanii 202 walipojiunga na  na mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki katika warsha ya kuwajengea uwezo wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza leo.
 Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniiwaliojiunga na  PPF kupitia mfumo wa Wote Scheme.
 Msanii wa filamu  Mwanaharusi Hela akizungumza jinsi alivyofurahishwa na  mfumo wa wote scheme kupitia PPF ambapo utamnufaisha kwa kupata huduma ya afya  na mkopo wa maendeleo.
 Msanii na mpiga picha wa filamu akichangia maada wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasanii wa Mikoa ya kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza.
 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi mwenye tisheti nyeupe akitoa maelekezo jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari wa PPF (Wote Scheme) ambapo PPF iliweza kutoa semina kwa washiriki umuhimu wa kuchangia na Mfuko wa Pensheni wa PPF.

 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi  kulia akitoa maelekezo kwa wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza. 
 Msanii akijaza fumu ya kujiunga na uanachama wa mfuko wa PPF jijini Mwanza mara baada ya kuhudhuria warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasanii hao jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.