Kufungwa kwa Mageti ya Daraja la Kigamboni Kwasababisha, Vurugu, Foleni
DAR ES SALAAM: Kufungwa kwa muda kwa mageti mengi ambayo hutumiwa na magari kupita katika Kivuko cha Daraja la Nyerere (Kigamboni) leo Novemba 7, 2016 na mamlaka husika na kuacha geti moja tu litumike kwa magari yote, kumesabaisha vurugu na foleni kubwa ya magari kivukoni hapo.
Daladala, lori na magari madogo yakiwa kwenye foleni ili kupita kwenye geti moja.
Katika kivuko hicho ambacho kina mageti mengi ambapo kila geti hupitisha magari; geti moja magari makubwa, jingine magari madogo, jingine daladala na kadhalika hivyo kufanya shughuli ya kupita magari kuwa rahisi.
Lori likiwa kwenye foleni moja na magari madogo.
Leo hali ilikuwa tofauti baada mageti hayo kufungwa huku likiachwa geti moja tu ambalo hata hivyo halikutosha kupitisha magari makubwa, madogo, daladala na bajaji kwa pamoja, hali hiyo iliamsha hasira kwa abiria wa daladala na watumiaji wengine wa kivuko hicho waliokuwa na magari yao binafsi wakivuka ng’ambo baada ya kuona hali hiyo ya kucheleweshwa kwa maksudi kwa kufungiwa mageti.
Mmoja kati ya abiria hao (hakutaka jina lake litajwe) waliokuwa wamekwama kivukoni hapo kutokana na tatizo hilo alihojiwa na mwanahabari wetu na kueleza haya;
“Binafsi nashangaa hawa jamaa wanafunga mageti kwa sababu ipi wakati ni wajibu wao kuhakikisha wapo kwenye haya mageti na magari yanapita kwa utaratibu uliwekwa, sasa wamesababisha foleni isiyokuwa ya lazima na kutuchelewesha makazini na kwenye mihangaiko yetu, kama wameshindwa kusimamia hapa waondoke waletwe watu wengine.” Abiria huyo alizungumza kwa hisia.
Foleni yabajaji na magari madogo.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wanaosimamia kivuko cha daraja hilo alipopata taarifa za tukio hilo aliwasili eneo la tukio na kuongea na baadhi abiria wa daladala na wenye magari binafsi huku akiwaomba msamaha kwa kilichotokea japo hakueleza kwa nini mageti hayo yalifungwa.
Kiongozi huyo akizungumza baada ya kuwasili eneo la tukio, nyuma likiwa geti limefungwa.
Abiria hao walionekana wenye hasira na kuendelea kumgombeza jambo lililosababisha aamuru mageti yote yafunguliwe na kuyaruhusu magari kupita na kendelea na safari zake.

No comments:
Post a Comment