Trending News>>

Dada Annie Nyaga: Bilionea kwa kilimo cha matikiti

Kilimo kinaonekana kuwa kazi ya watu wasio na elimu.Lakini mwanadada kutoka kenya amevunja dhana hiyo.

Annie Nyaga, msomi wa Bachelor’s degree in Biomedical Science and Technology ambaye ni mkulima wa mboga mboga na matunda.Ingawa alipata fursa ya ufadhili wa masomo ya master katika Biomedical Science and Technology Marekani baada ya kumaliza digirii ya kwanza hakwenda bali alijikita katika kilimo.

Anasema "Kilimo ndio ndoto yangu nilipoteza miaka minne katika chuo kikuu, Kilimo ndio kazi ninayopendelea kuliko nyingine yoyote.

Akiwa na miaka 28 tu amefanikiwa sana katika kilimo maeneo ya Mbeere, Embu County, ambapo analima matikiti, nyanya n.k.

Safari yake ilianza 2009 miaka miwili baada ya kumaliza digrii yake kwa mtaji wa 20,000KSh (1,400,000Tsh wakati huo).Alianza kwa kilimo cha French beans na baby corns lakini alipata hasara kubwa kutokana mfumo wa soko.

Licha ya changamoto hiyo hakukata tamaa bali aliongeze bidii na alianzisha kilimo cha matikiti ambacho anaendelea nacho mpaka leo, amefanikiwa sana katika la embu county

Leo hii Annie anawafanyakazi kadhaa na avuna 30tonnes na anauza 28Ksh per kilo, na kupata faida ya 600,000Ksh(sawa na 12,000,000Tsh) kwa miezi mitatu ya kuvuna matikiti pekee.

No comments:

Powered by Blogger.