Trending News>>

Vigezo vya utoaji wa mikopo elimu ya juu vyawekwa

Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, imetoa vigezo vipya vya kukopesha wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini kugharimia masomo yao.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Naibu waziri wizara ya elimu sayansi na tekinolojia Mhandisi Stella M. Manyanya amesema kuwa Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo ikiwemo Vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano,

Amesema kupitia mpango wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele kama vile Fani za Sayansi za Tiba na Afya,Ualimu wa Sayansi na Hisabati, Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu

Akitaja vigezo hivyo Mhandisi Manyanya amesema utoaji wa mikopo utazingatia Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile Ulemavu na Uyatima , Ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri na kuongeza kuwa kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (katika vipengele vyote vya mikopo.

No comments:

Powered by Blogger.