Unasoma Hadi PHD Hujawahi Kufanya Kazi, Una Matatizo – Mwijage
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewachana vijana wanaotumia miaka mingi kuwa chuoni wakisoma hadi kufika kiwango cha PHD bila kupitia ujuzi wa kazi yoyote.
Ameyasema hayo Jumatatu hii katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV akidai kuwa vijana wengi wanapenda elimu aliyooita ya ‘mseleleko’ akimaanisha elimu ya moja moja kwa moja bila ya kujaribu kufanya kazi yoyote au bila kupitia ujuzi mbalimbali wa kazi.
“Tatizo moja tulilonalo tunapenda elimu mseleleko,” alisema. “Sipendi kuizungumzia elimu lakini nataka niseme tunapenda elimu mseleleko, yaani unaanza leo miaka 6 unaanza darasa la kwanza, unakwenda moja kwa moja mpaka unamaliza PHD,hujawahi kufanya kazi. Mimi sikusoma elimu mseleleko na ndiyo maana mimi watu wengine kama ntalisema hili wengine litawaudhi shauri yao,” alisisitiza.
“Watu wengine wanapenda kujua mimi nimesoma shule gani, kimsingi mimi elimu ya darasani ni ndogo, niliyonayo ni elimu ya mtaani nimefanya kazi nyingi, mi nimevua samaki, nimefanya kazi gereji, ukiniuliza naweza nikakuuliza ukasema na hili Mwijage unalijua. Mimi nilikuwa hata Dj nilikuwa MC, nimefanya kazi nyingi sana kwenye field,nimepiga debe mimi, kwahiyo mimi vitabu vya darasani sina,” alieleza.
“Lakini hii elimu mseleleko hii hujawahi kufanya kazi yoyote unakuwa injinia hujawahi kusimamia hata jengo moja ina matatizo. Kwahiyo vijana mkikwama tafuta namna ya unavyoweza kuanza. Mi nawafahamu watu ambao waliokwenda kusoma kutokana na vipato walivyojitafutia,mi nawafahamu watu waliofanya vibarua kujilipia karo.”
“Sasa mtu anasoma kuanzia darasa kwanza moja kwa moja mpaka PHD bila kufanya kazi yoyote, hata vijana wa Ulaya mbona wanafanya kazi wanajilipia karo, so we have problem kwasababu ni maskini tunapenda kwasababu ya kupenda haya ya mseleleko. Mtu akianza wenzake wakimtangulia aliokuwa anasoma nao anajisikia vibaya. Mi mbona kuna watu tulimaliza nao form six wakaenda chuo kikuu na mimi sikuenda nilikuwa nafanya mambo mengine!
No comments:
Post a Comment