PSG wamtafuta Neymar kwa euro milioni 222
Klabu ya soka ya Paris Saint-Germain imesema kwa sasa lengo lao ni
kumnasa mshambuliaji wa Barcelona Neymar Jr soko litakapofunguliwa
majira yajayo ya joto.
Mabingwa hao wa Ufaransa wako tayari kuweka mezani dau la euro milioni
222 kwa ajili ya raia huyo wa Brazil, kiasi ambacho kitawafanya wampate
kutokana na kipengele cha kumwachilia huru kilichopo kwenye mkataba wake
na Barcelona, kwa mujibu wa tovuti ya Goal.com
Goal wameripoti kwamba, vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vimethibisha
kwamba uhamisho huo ulikaribia kukamilika hadi pale Neymar alipoamua
kusaini mkataba mpya na Barcelona.
PSG wanatarajia kurudi tena kwa mchezaji huyo mara baada ya msimu huu kukamilika.
Iwapo juhudi za kumsajili Neymar zitafanikiwa, nyota huyo atakuwa
akilipwa mshahara sawa na ule anaolipwa nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Mkataba mpya wa Neymar unaomalizika 2021 una thamani ya euro milioni 25
kwa mwaka mbali zaidi na ule wa Messi wenye thamani ya euro milioni 42
kama mshahara wake wa mwaka mzima.
Endapo Neymar atahamia Paris, ataungana na ndugu zake wa Brazil
Marquinhos, Lucas Moura pamoja na Thiago Silva kwenye mji huo mkuu wa
Ufaransa.
No comments:
Post a Comment