ACT Wazalendo yaiomba serikali majibu ya maswali haya mawili
ACT Wazalendo yaiomba serikali majibu ya maswali haya mawili
Chama cha ACT Wazalendo kimestushwa Na taarifa kwamba Nchi yetu inabadilisha msimamo wake kuhusu
Sahara Magharibi. Tumepata Taarifa kwamba Mfalme wa Morocco
ataitembelea Tanzania Hivi karibuni Na kusaini mikataba mbalimbali ya
biashara Na Nchi yetu Kwa ahadi kwamba Nchi yetu utaiunga mkono Morocco
katika kuifukuza Jamhuri ya Sahrawi kutoka Umoja wa Afrika.
Chama chetu kinaomba ufafanuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje juu ya masuala yafuatayo:
• Ni kweli msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi umebadilika?
• Tanzania itaendelea kuitambua Jamhuri ya Sahara Kama dola Huru Na kulinda kiti chake katika AU?
Sisi ACT Wazalendo tunatangaza dhahiri kwamba hatutaunga mkono kuvunjwa
Kwa Msingi Mkuu wa Sera ya Mambo ya Nje ya Nchi yetu ya kusimama Na
wanyonge.
Iwapo Serikali itathubutu kuipa mgongo Jamhuri ya Sahara, tutahamasisha
wanachama wetu Na Watanzania wengine wenye kuheshimu harakati za
ukombozi kufanya MAANDAMANO Siku mfalme wa Morocco anaingia Nchini.
Kamati ya Mambo ya Nje ya ACT Wazalendo imeandika barua Kwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba
kikao naye ili kupata ufafanuzi wa kina kuhusu suala la SAHRAWI.
John Patrick MbozuKatibu, Kamati ya Mambo ya Nje, ACT Wazalendo
No comments:
Post a Comment