Yanga kumenoga Manji atangaza kurejea tena...
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji rasmi ametangaza kuwa yupo tayari kurejea kuiongoza klabu hiyo ikiwa ni muda mrefu kidogo toka atangaze kujiuzulu nafasi yake ya umwenyekiti ndani ya klabu hiyo.
Taarifa hiyo imeandikwa Afisa habari msaidizi wa klabu ya Yanga Sc Godlisten maarufu kama “Zechicharito” kupitia ukurasa wake wa instagram yenye maneno yanayosomeka hivi.
“ Yanga ni klabu yetu sote na binafsi hii ni kama sehemu ya familia yangu. Kuiona klabu inasuasua kiasi hiki sifurahi”
“ Wapo waliotufikisha hapa lazima wawajibike kwa mizani ya uongozi bora ili sote tuungane kuijenga upya klabu katika misingi bora na endelevu”
“Misingi Endelevu ili yoyote yule mwenye mapenzi mema na klabu, weledi katika uongozi aweze kuiongoza”
“ Binafsi sina pingamizi kurejea endapo watawajibika waliotuvuruga , wanachama kuridhia kuijenga Yanga mpya yenye mtazamo chanya kimaendeleo uwanjani na miundo mbinu bora katika dhana nzima ya nguvu za kiuchumi”
YUSUFU MANJI
Mbali na hilo zipo taarifa zilizotufikia sokaonline kuwa asilimia kubwa ya matawi yote ya Yanga Sc yaliyopo kwenye mikoa tofauti yamekubaliana kumuachia bosi huyo kununua hisa ndani ya klabu hiyo na kwa pamoja wamepanga siku ya mkutano Jumapili hii June 10, 2018 kuingia na kauli mbiu ya “MABADILKO NA MANJI”
No comments:
Post a Comment