Xavi, Raul, Xabi na Victor Valdes pamoja na wengine wengi wamehitimu mafunzo ya Ukocha..
Nyota wanne waliyopata kuitumikia timu ya taifa ya Hispania wamekuwa miongoni mwa wachezaji 16 waliyo tunukiwa vyeti vya ukocha na UEFA baada ya kupata mafunza kwa muda wa wiki sita.
Wachezaji hao wazamani wa Hispania ni Xavi, Raul, Xabi Alonso na Victor Valdes huku wengine waliyopata vyeti hivyo ni pamoja na winga wazamani wa Liverpool, Albert Riera na aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal, Julio Baptista wamefanikiwa kuhitimu kozi hiyo leo siku ya Ijumaa majira ya asubuhi.
Mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo sasa wanaweza kuanza na timu za vijana na baada ya mwaka mmoja wataweza kupatiwa leseni na UEFA.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania, Alonso na Raul wote wamepatiwa ofa ya kufundisha kikosi cha vijana cha Real Madrid msimu ujao.
Miongoni mwa mabo waliyofundishwa ni pamoja na Utawala bora, maswala ya lishe, Saikolojia, Madawa, namna ya kuitengeneza timu na mengineyo.
No comments:
Post a Comment