Trending News>>

Wakala wa Mo-Salah apewa dili la Salah kujiunga na Barcelona

Ikiwa tayari zimesalia siku 7, kuingia kwa michuano ya Kombe la Dunia, lakini mawakala wote Duniani wanahaha kusaka timu mpya za waajiri wao. Hali kadhalika wakala wa Salah yupo kazini.


Wakala wa Mohamed Salah yupo nchini Hispania kuangalia fursa ya mwajiri wake kujiunga na miamba ya Catalunya Barcelona.


Chombo cha Habari nchini Hispania, AS, kimeripoti kufanyika mikutano kadhaa za kumfanya staa wa Liverpool kwenda Barcelona kukiwa na nafasi ya kujiunga na miamba hiyo.


Salah, 25, alikuwa katika kiwango kizuri msimu huu ulioisha akiwa amefunga goli 44 katika jumla ya michuano yote Ulaya. Liverpool walimsajili Salah kutoka As Roma kwa pauni milioni 36.9 ambazo Barcelona wapo tayari kurudisha.


No comments:

Powered by Blogger.