Trending News>>

UFAHAMU MPIRA UTAKAOTUMIKA KWENYE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI.


Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea kwenye michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, leo tuchambue mpira utakaotumika kwenye mashindano hayo.
TELESTAR 18.
Mpira huo ndo utakaotumika kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia.
Mpira huo umetengenezwa na kampuni ya Ujerumani,  ambayo inatengeneza vifaa vya michezo vya Adidas.
Mpira huo ulitengenezwa mwaka 1970, unaitwa Telestar ulianza kutumika katika fainali iliyofanyika nchini Mexico.
Mpira huo unauzwa Dolla za Kimarekani 100 ambazo ni sawa na shilingi 2,2700 za Kitanzania.
Mpira huo umetengenezwa katika kiwango cha hali ya juu na ubora ukifananishwa na mpira uliotumika kombe la dunia Mwaka 1970.
Mpira umewekewa miscrope ndani yake ambayo inaweza kuongeza spidi ya mpira na una uwezo wa kufika mbali ukipigwa hewani.
Kama ulikuwa hufahamu, Adidas  ndio mpira wa pili kutengenezwa katika michuano ya kombe la dunia.
Mpira wa kwanza ulitengenezwa mwaka 1970, ulitengenezwa na rangi nyeupe na nyeusi,  ili iweze kuwasaidia mashabiki watakaotizama kupitia runinga waweze kuona mpira kirahisi kwa sababu zamani runinga zilizokuwa zinaonyesha rangi nyeupe na nyeusi.
Nakumbusha kidogo Fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Mexico, mpira uliotumika ulikuwa unaitwa Telestar,  na mpira utakaotumika mwaka huu 2018 unaitwa Telestar 18.

No comments:

Powered by Blogger.