Sababu za Leroy Sane kuachwa Kombe la Dunia..
Mwaka jana wakati Guardiola akiwaza namna ya kumtumia Jesus Navas, akili yake ilimwaminisha kwamba Navas ahafai kwenye mipango yake. Mwisho wa siku ilibidi wacheze kamari ya Euro milioni 38 kwa ajili ya Leroy Sane.
Guardiola amefanikiwa kabisa kwa kamari yake ya msimu wa kwanza.Sane amefanya vyema sana msimu wa kwanza. Kwanza alichomfurahisha sanna Pep ni uwezo wa Sane kuelewa kiingereza vizuri sana na kwa mapema. Sane ameonekana mara nyingi akiwasiliana na wenzake bila tabu yoyote na amekuwa na uwezo kukwepa majeraha na mara alipopata majeraha alirudi mapema.
Akiwa na miaka 22 amemaliza msimu wake wa kwanza kwa mabao 14 na kuasisti mabao 19 katika michezo 49.
Baadhi ya waandishi wa habari wamemfananisha Sane maraka kadhaa na staa wa Man United Ryan Giggs kwa namna wanavyocheza. Mwaka wake wa kwanza amefanikiwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka PFA. Joachim Low bado anaamini mfumo wake haumhitaji Sane.
Sane mwezi Januari mwaka huu alitania kwamba kama watashinda kombe la Dunia atastaafu soka. Mambo sio Mambo mbali na kujiandaa vizuri hadi kwa kubadilisha aina yake ya nywele lakini bado kura zake hazikutosha.
Low anasemaje
Hajafika katika mechi za kimataifa bado, lakini nilipata wakati mgumu kugundua yupi bora kati ya Julian Brandt na Leroy Sane.
Kikosi cha Die Mannschaft wanajiandaa kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo kama ilivyokuwa kwa Brazil mwaka 1962.
Low binafsi naona kama amefanya uamuzi mkubwa na mgumu sana. Mwanzo walio wengi walilaumu kuachwa kwa Mauro Icardi lakini hili la Sane binafsi ni kama lina uonevu mkubwa usio na mantiki.
Anasema kwamba Sane amelingana uwezo na Brandt naona kama ni matusi. Sane amehusika mabao 33 hakuna mchezaji yeyote wa Ujerumani mwenye takwimu hizi za Sane.
Michael Ballack mwenyewe anakiri kwamba Low amejiweka katika wakati mgumu na presha kubwa kwa kumuacha mchezaji aliyeng’ara msimu mzima.
Mwandishi nguli wa Mirror Bwana Alex Richard ametoa mawazo yake
Kwanza Ujerumani wana upungufu mkubwa wa wachezaji muhimu kwa baadhi ya nafasi hasa kwa kuangalia wachezaji wazoefu. Wanamkosa Emre Can, Shkrodan Mustafi na Mario Gotze, ambao wote walikuwepo kwenye kikosi cha ubingwa mwaka 2014.
Hili wala sipingani nae kabisa. Kwa ubunifu alio nao Sane sio mchezaji mwenye flo nzuri ya mpira kama ya Sane labda Reus. Ozil anaweza kukaa na mpira lakini hana kasi kama ya Sane. Yaani leo hii kama Sane angekuwa muingereza kila koma kila faulo hata goli kiki waingereza wangemtaka apige hasa kwa ubunifu wake na uwezo wa mguu wake wa kushoto.
Hebu angalia tu, Hakuna Sandro Wagner, mwenye magoli matano kwenye mechi 8 za timu ya taifa na pia kiungo Serge Gnabry hatokuwepo kikosini. Hilo benchi laoina watu gani sasa?
Sane amekuwa na msimu mzuri sana na amecheza ligi ngumu na yenye ushindani. Mfumo wa Low ni 4-2-3-1. katika mfumo huu Thomas Muller atatokea upande wa kulia na Mesut Ozil atacheza namba 10 na sehemu iliyobakia ni ya kushoto ambako Sane anacheza. Katika sehemu ya kushoto imechukukiwa na Marco Reus ambaye alikosa Kombe la Dunia mwkaa 2014 na Kombe la Yuro 2016.
Ni mchezaji ambaye amekuwa akikumbwa sana na majeraha. Amecheza michezo 11 kati ya 13 ya Mwisho ya Borussia Dotmund tokea alipotoka Majeruhi mwezi desemba mwaka jana. Reus katika michezo hiyo 11 amefunga mabao 7.
Kwa upande wangu ninawaza pia, Ujerumani itakosa mchezaji mwenye uwezo wa kukaa na mpira na kupunguza mabeki kadhaa katika benchi lake. Sane alikuwa mchezaji mbadala pale Reus atakaposhindwa au ozil kuchoka
Low ni kipenzi cha Julian Draxler
Julian Draxler, ana miaka 24. amekuwabkwenye wakati mgumu sana tokea Neymar ajiunge na mabwenyenye wa PSG. Draxler amecheza michezo 40 msimu kwa klabu ya PSG licha ya ufinyu mkubwa wa namba .
Draxler alikuwa nahodha kwenye michuano ya Confederation ambapo timu ilibeba kombe hilo nae kuibuka na kiatu cha dhahabu.
Mpinzani mkubwa wa Sane kijana Brandt amefunga magoli 12 na kutoa asisti 7 katika michezo 39 lwa klabu yake ya Bayer Leverkusen. Brandt amekuwa na uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa tokea 2016, anajituma sana kukaba na ana uwezo wa kubadilisha nafasi moja hadi nyingine.
Sane amekuwa na mambo mengi mno. Katika michuano ya confederation alijittoa kwenge kikosi ili kwenda kufanya uchunguzi wa pua tatizo ambalo ilionekana kuwa dogo na angeweza kujitoa tu kwa taifa lake.
Katika michezo 12 ametengeza bao moja peke na hajafunga bao lolote kwa taifa lake. Amekuwa mzuri kwenye mifumo ya Guardiola kwa kuwa ana muda mwingi wa kukaa nae mazoezini na kumwelekeza kitu cha kufanya. Naona kama Low hana muda kusumbuka kumweka mchezaji mpya kwenye mfumo wake kwa kulazimisha au kwa kuriski.
Licha ya kwamba nadhani mwalimu mwenyewe ndiye aliyeshindwa kumtumia Sane. Ni kazi ya mwalimu kuhakikisha mchezaji bora anaingia kwenye mfumo wake
Kikosi chao
Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Marc-Andre Ter Stegen (Barcelona/ESP), Kevin Trapp (Paris Saint-Germain/FRA)
Walinzi: Marvin Plattenhardt (Hertha Berlin), Jonas Hector (Cologne), Matthias Ginter (Moenchengladbach), Mats Hummels (Bayern Munich), Niklas Suele (Bayern Munich), Antonio Rudiger (Chelsea/ENG), Jerome Boateng (Bayern Munich), Joshua Kimmich (Bayern Munich)
Viungo: Sami Khedira (Juventus/ITA), Julian Draxler (Paris Saint-Germain/FRA), Toni Kroos (Real Madrid/ESP), Mesut Ozil (Arsenal/ENG), Thomas Mueller (Bayern Munich), Sebastian Rudy (Bayern Munich), Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Ilkay Gundogan (Manchester City/ENG), Leon Goretzka (Schalke 04), Marco Reus (Borussia Dortmund)
Washambuliaji: Timo Werner (RB Leipzig), Mario Gomez (VfB Stuttgart)
No comments:
Post a Comment