Trending News>>

Nyota Simba kuikosa GorMahia

Kiungo mshambuliaji wa Simba Haruna Niyonzima hatacheza mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kesho dhidi ya Gor Mahia kwa kuwa ana kadi mbili za njano.

Kulingana na kanuni za michuano hiyo, mchezaji mwenye kadi mbili za njano atakosa mchezo mmoja.


Kaimu Kocha wa Simba Masudi Djuma amesema ana wachezaji 18 hivyo kukosekana kwa Niyonzima hakuwezi kuwa tatizo.


Kesho Jumapili ya June 10 majira ya saa 15:00 alasiri Simba itashuka dimbani kuwavaa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Gor Mahia kwenye uwanja wa Afraha Mjini Nakuru, Kenya.


No comments:

Powered by Blogger.