Trending News>>

Mwanamke aandika CV kwenye mtandao kutafuta Mchumba

Kwa sababu ya kuwa peke yao, baadhi ya wanawake wameamua kutafuta waume katika mitandao ya kijamii.


Binti mmoja mrembo aliamua kufanya hivyo ambaye Jumamosi, Juni 2 katika mtandao wa Twitter aliandika mambo mema kujihusu kwa lengo la kupata mchumba.


Msichana huyo, kwa jina Ogoo (@ogochukjennifer) katika mtandao wa Twitter, alieleza kuwa anaweza kupika vizuri, huwa anatia bidii kazini, ni mrembo na ana umbo la kuvutia.


Ogoo aliwaomba wafuasi wake kusambaza ujumbe huo kwa sababu huenda mchumba wake alikuwa katika kurasa zao.


Binti huyu anahitaji mchumba. Picha/Ogochukjenniffer/Twitter

Aliandika, “Twitter fanya jambo, ninahitaji mpenzi, ninaweza kupika, ninafanya kazi, mimi ni mrembo na nina umbo la kuvutia. Naomba mueneze, labda mpenzi wangu yumo katika kurasa zenu. Na mimi sio bintiye Chimamanda. Asantenti,” aliandika.


Binti huyu anahitaji mchumba. Picha/Ogochukjenniffer/Twitter

No comments:

Powered by Blogger.