Trending News>>

Babu Tale abadili Gia angani kwa Zari...South....

Akizungumza na mtandao wa Dizzmonline na kuliambia kuwa, klichompeleka Afrika Kusini kwa Zari sio kumshawishi arudiane kimapenzi na Diamond, ila yeye ameenda kuhakikisha kuwa wawili hao wanamaliza matatizo yao ili waweze kuzingatia suala la kulea watoto kwa pamoja,na amesisitiza kuwa kama Zari na Diamond wataamua kurudiana kimapenzi utakuwa ni uamuzi wao wenyewe.




Dar es Salaam. Baada ya mashabiki na watu wa karibu wa Zari na Diamond, kusubiria jibu la Meneja wa Diamond, Babu Tale  kurudisha penzi la Zari ‘The boss Lady’ na Nasib Abdul ‘Diamond’ ameibua mpya.
Akizungumza na mtandao wa Dizzmonline na kuliambia kuwa, klichompeleka Afrika Kusini kwa Zari sio kumshawishi arudiane kimapenzi na Diamond, ila yeye ameenda kuhakikisha kuwa wawili hao wanamaliza matatizo yao ili waweze kuzingatia suala la kulea watoto kwa pamoja,na amesisitiza kuwa kama Zari na Diamond wataamua kurudiana kimapenzi utakuwa ni uamuzi wao wenyewe.
Babu Tale Juni 2, 2018, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea namna atakavyorudisha penzi hilo ambalo kwa maneno yake anaona kama kumsukuma mlevi vile.
Kumbuka Zari aliwahi kufanya mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza la BBC Swahili na kusema kuwa hawezi kurudiana na Diamond licha ya wawili hao kuonekana kuwa bado wanapendana.
Babu Tale ameyasema haya kupitia ulimwengu wa Instagram ambao sasa hivi kwa Watanzania ni kama ndio sehemu yao ya kushinda.
“Naona watu mnaniandikia meseji niwarudishe Mr and Mrs Dangote, hili kwangu ni kama kumsukuma mlevi yani kazi ndogo sana, ila Niliwaacha tu kwanza kila mtu sumu na hasira za mioyo yao ziwaishe ili wakirudiana akili iwakae sawa.
“Sasa naona muda muafaka wa kulitumia jina langu ipaswavyo, kama ambavyo mama Tee ananiita “Godfather”, siendi na magoti wala kutambaa. Nitapanda ndege kwenda hadi SA kuongea na mtu mzima mwenzangu na ninaamini yataisha kwa asilimia 100, wananzengo niende nisiende?”
Baada ya kuandika hivyo, siku ya pili Babu Tale picha na video zilimuonesha katika ukurasa wake wa Instagram akisema yupo tayari kumaliza mgogoro huo na anaonekana yupo Airport kuelekea Afrika Kusini.
Pia, hakuishia hapo, hata alipofika Afrika Kusini akipofika, alituma video akiwa anakula na Zari huku akisema amefika na anahitaji maombi ya watu ili Zari akubali, ila siku ya pili akatuma picha tena na kusema kuwa watu waombe Mungu kwani amefanikiwa asilimia 50 bado 50.


No comments:

Powered by Blogger.