Trending News>>

NI SIMBA AU YANGA TAIFA LEO?



Watani wa jadi Simba na Yanga wanashuka dimbani jioni ya leo katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara, ikiwa ni mzunguko wa pili au lala salama wa michuano hiyo.
Vikosi vyote viwili tayari vimesharejea Dar es Salaam kutoka Morogoro ambako viliweka kambi kwaajili ya kujifua na mtanange wa leo, unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la taifa jijini Dar es Salaam, ambapo mchezo huo unategemewa kuwa wa kukata na mundu.


Kikosi cha wachezaji wa Simba

Mchezo wa leo utakuwa mtihani wa kwanza kwa kocha mpya wa Yanga, Mkongo Mwinyi Zahera, ambaye amechukua mikoba ya Lwandamina aliyeikacha timu hiyo na kurejea timu yake ya zamani ya Zesco United ya nchini Zambia, hivyo Zahera leo atataka kuonyesha kuwa yeye ni chaguo sahihi kwa Yanga.
Kwa upande wa kocha Mfaransa wa Simba, Pierre Lechantre, yeye hana presha kubwa maana amekuwa na kikosi chake kwa muda mrefu na tayari ameshawazoea wachezaji wake, hivyo kumfanya kutopata shida sana katika kupanga kikosi cha leo.

Kikosi cha wachezaji wa Yanga

Simba na Yanga zinaingia uwanjani siku ya leo zikiwa na tofauti ya pointi 11, ambapo Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 59 mara baada ya kushuka dimbani mara 25, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 48 mara baada ya kushuka dimbani mara 23.

No comments:

Powered by Blogger.