Kutoka Nike mpaka Toyota: Mikataba 31 inayomfanya Ronaldo kuwa mwanamichezo tajiri zaidi duniani
Cristiano Ronaldo ndio mwanamichezo ambaye ana mvuto wa kibiashara kuliko yoyote duniani kutokana na deals nyingi za kibiashara alizonazo nahodha huyo wa Ureno.
Kiujumla – mshindi wa mara 5 wa Ballon d’Or ana mikataba 31 na makampuni ya biashara duniani, mikataba hii inamfanya kuwa mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi zaidi katika ulimwengu.
Haijalishi ni sekta ipi – brands kubwa duniani zinapendwa kujihusisha na mwanasoka huyu, makampuni kutoka kaskazini mwa Afrika, Marekani, Japan, Ulaya na kwingine – kote utamkuta CR7.
Ingawa hakuna namba rasmi ya mikataba yake mingine – lakini Mkataba mkubwa kabisa wa Ronaldo unaripotiwa kuwa mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike – kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali – CR7 anaingiza benki kiasi cha paundi millioni 21 – sawa na zaidi ya billioni 75 kwa mwaka – mkataba huu anao kwa maisha yake yote, anaungana na Lebron James na Michael Jordan kuwa watu pekee wenye mikataba ya maisha na Nike.
Kampuni ya kiingereza ya Castrol inayojihusishi na utengenezaji wa mafuta vilainishi, oils za magari, na vifaa vingine vya moto – ni kampuni nyingine ambayo imemtumia na inaendelea kumtumia Ronaldo katika matangazo yake ya biashara, mwaka 2009 alisaini nao mkataba wa miaka 2 uliokuwa na thamani ya £8.5m – sawa na zaidi ya billioni 25 za kitanzania. Mwaka jana Ronaldo aliongeza tena mkataba wake na Castrol japo taarifa za malipo ya mkataba huo bado hazijatolewa.
Kampuni ya mawasiliano ya ZTE alijiunga na listi ya makampuni ya biashara yanayofanya kazi na Ronaldo na wanaripotiwa kumlipa kiasi cha £3m kwa mwaka (zaidi ya billioni 10 za TZ).
Akiwa na miaka 33 akielekea ukingoni mwa maisha yake ya soka – CR7 bado anaendelea kuvutia makampuni makubwa – Toyota ni kampuni nyingine iliyojiunga na brand ya CR7 hivi karibuni – na dili linamhakikishia nafasi ya kwanza tena katika listi ya wanamichezo wanaolipwa vizuri zaidi duniani.
Forbes waliripoti kwamba kwa mwaka 2017 – Cristiano Ronaldo aliingiza bank kiasi cha $93m – sawa na zaidi ya billioni 220 za kitanzania.
Jarida hili linaripoti kwamba $58m kutoka kwenye fedha hizo zimetoka na mshahara na bonasi kutoka Real Madrid na nyingine zimetoka na malipo ya udhamini wa makampuni ya biashara na biashara zake nyingine binafsi!
LISTI YA MAKAMPUNI YA BIASHARA YANAYOFANYA KAZI NA RONALDO
Coca Cola, KFC, video games maker Konami
Emirates Airline
Banco Espirito Santo
Castrol Oil & petrol
Emporio Armani
Soccerade Sports drink
Herbalife Supplements & sports nutrition,
JBS Clothing (retail)
Samsung Consumer electronics
Jacob and Co. Fashion
TAG Heuer Watches
Clear Shampoo Cosmetics & toiletries
Sportlobster
MTG Pharmaceutical
PokerStars.com
Abbott Laboratories
Altice
ZTE
Smaaash Entertainment
XTrade
Exness Brokerage & consulting
PanzerGlass
Egyptian Steel
American Tourister
Toyota
No comments:
Post a Comment