Jupp Heynckes kuendelea kufukuzia rekodi nyingine ya makombe 3 hii leo
Hii leo nchini Ujerumani kutakuwa na pambano kubwa lingine, Bayern Leverkusen watakuwa nyumbani kwao kuikaribisiha Bayern Munich katika jaribo la kocha Jupp Heynckes kubeba makombe matatu tena.
Heynckes tayari ametabiri kwamba Leverkusen ndio watakuwa wapinzani wakubwa wa Bayern Munich katika Bundesliga msimu unao, hii ni kutokana na ubora wao siku za usoni lakini hii leo wanakutana kwanza katika nusu fainali ya DFB Cup.
Leverkusen wanakutana na Bayern Munich huku uwezo wao wa kuwakabili Bavarians ukiwa ni swali kubwa miongoni mwa watu, katika mechi mbili zilizopita katika Bundesliga Leverkusen wamefungwa zote na Munich.
Mara ya mwisho timu hizi mbili zilikutana katika michuano hii katika robo fainali ya mwaka 2015, katika mchezo huo dakika 120 zilimalizika kukiwa hakuna mbabe. Mikwaju ya penati iliwapa ushindi Bayern kwenda nusu fainali.
Mwaka 2009 wakati huo hadi Artulo Vidal alikuwa akiichezea Bayern Leverkusen ilikuwa mara ya mwisho kwa Leverkusen kuwafunga Munich katika michuano hiyo wakiibuka kidedea cha mabao 4-2.
Mwaka 1993 ndio mara ya kwanza na mwisho kwa Leverkusen kubeba ubingwa wa DFB lakimi wapinzani wao Bayern Munich wenyewe wana rekodi ya kubeba kombe hili kwa mara 18 hadi hivi sasa.
No comments:
Post a Comment