Road To World Cup “Fifa waitosa rasmi Uingereza kombe la dunia”
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1938 michuano ya kombe la dunia itapigwa bila kuwepo muamuzi kutoka katika nchi ya Uingereza, hii ni baada ya Fifa kutoa taarifa rasmi.
Tayari waamuzi 36 kutoka maeneo mbali mbali duniani watakaochezesha michuano hiyo wameshatajwa lakini hakuna muamuzi kutoka nchini Uingereza, Scotland, Ireland wala muamuzi kutoka Wales.
Muamuzi pekee ambaye alikuwa apate nafasi kutoka Uingereza ni Mark Clattenburg ambaye hata hivyo aliachana na ligi hiyo kubwa na kwenda kufundisha soka ligi ndogo Saudi Arabia jambo lililomyima fursa kuwepo katika kombe la dunia.
Hata hivyo chama cha soka nchini Uingereza FA kiliwaomba FIFA kama wanaweza kuweka jina la kocha mwingine kutoka Uingereza kuchukua nafasi ya Clattenburg lakini chama hicho cha soka duniani kililikataa ombi hilo.
Sio muamuzi wa kati tu bali FIFA pia imewatosa Uingereza katika orodha ya marefa wa ziada 63 huku hii pia ikiwatoa Uingereza katika orodha ya marefa ambao watakuwa wakisimamia teknolojia ya maamuzi ya video (VAR).
Mwaka 2010 ulikuwa nchini Urusi fainali kati ya Hispania na Uholanzi ilichezeshwa na muamuzi wa Kiingereza Howard Webb lakini sasa taifa hilo linaonekana kuyumba kiuamuzi suala lililopelekea FIFA kuwatosa. Orodha kamili ya waamuzi hii katika michuano hiyo hii hapa
No comments:
Post a Comment