Tanzania imepewa uenyeji mkutano mkuu wa FIFA
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA
utakaofanyika February 22, 2018 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa
wa Mwl. Nyerere Dar.
Mkutano huo utashirikisha jumla ya mataifa 19 wanachama wa FIFA huku
mwenyekiti wa mkutano akiwa ni Rais wa FIFA Gianni Infantino.
Miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa fedha za
FIFA kwa ajili ya maendeleo ya soka, changamoto za usajili kwa njia ya
mtandao Transfer Matching System (TMS).
Rais wa TFF Wallace Karia wakati akitangaza kufanyika kwa mkutano huo
amesema, ni heshima kwa Tanzania na TFF kuwa mwenyeji wa mkutano huo
mkubwa wa shirikisho la soka Duniani.
“Tunamshukuru sana Mungu na FIFA pia kwa kututhamini na kutupa
uenyeji huu, ni faraja kubwa sana kwetu kupata nafasi hii”-Wllace Karia.
Mataifa yatakayoshiriki mkutano huo ni Tanzania (mwenyeji), Algeria,
Mali, Morocco, Burkinafaso, Angola, Niger, Bahrain, Palestina na Saud
Arabia.
Mengine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Tunisia,
Bermuda, Monserrat, St Lucia, Visiwa vya US Virgin, Maldives na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment