Barcelona waipiga bao Real Madrid katika maingizo ya haki za matangazo
Soka ni biashara na kwa wenzetu kila jambo linalofanyika
katika soka baasi wanajaribu kulitmia kuingiza kipato, suala la
matangazo ya video hutumika kwa kiasi kikubwa sana kuingiza kipato
katika vilabu vya Ulaya.
Klabu ya FC Barcelona wanaonekana kuingiza kiasi kikubwa cha pesa zinazotokana na matangazo ya Televisheni kuliko timu yoyote katika La Liga ambapo kwa msimu wa 2016/2017 Barcelona wamekusanya kiasi cha £146.2.
Real Madrid pamoja na kuchukua makombe lakini hawajawafikia Barcelona katika kiasi cha pesa kinachoingizwa kutokana na matangazo ya televisheni kwani Real Madrid wenyewe wameingiza kiasi cha £140.1m.
Pesa wanazopata Athletico Madrid zinawafanya kuwa nafasi ya tatu wakiwa wameingiza kiasi cha £99.2m wakifuatiwa na Athletic Club walioingiza £71m huku Valencia wakiweka mfukoni kiasi cha £67.4m.
Barcelona msimu huu umekuwa mzuri sana kwao ndani ya uwanja kwani hadi sasa wanaendelea kuongoza ligi wakiwa wamewaacha wapinzani wao wakubwa Real Madrid kwa alama 14.

No comments:
Post a Comment