AMRI SAID TUPO TAYARI KUIKABILI KAGERA SUGAR KESHO
Kocha mkuu wa timu ya Lipuli inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara Amri Said amebainisha kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar "Wanankurukumbi" utakaofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumamosi ya January 27.
Said amesema licha ya safari ndefu ya kutoka mkoani Iringa hadi Kagera lakini anaamini kuwa watapata muda mzuri wa mapumziko na ule wa kufanya mazoezi ili kuwa tayari kuchukua alama tatu mjini Bukoba.
"Tunashukuru Mungu tumefika salama Kagera, kinachotakiwa kwa sasa ni kuondoa uchovu wa safari, japokuwa miili yetu inafatiki lakini tutajitahidi kuuondoa uchovu," alisema Amri Said.
Mchezaji huyo wa zamani wa Lipuli na Simba, amesema hawataidharau Kagera Sugar kisa kupoteza michezo miwili mfulululizo kwani hiyo ni hali ya kawaida na ligi msimu huu imekuwa ngumu kwa kila timu kujiandaa vyema.
"Kagera sio timu mbaya, ligi ni ngumu kila mmoja anafahamu, hata sisi tumetoka kupoteza mchezo mmoja na kutoka sare mmoja, hivyo tunawaheshimu Kagera naamini kabisa watakuwa vizuri kimpira watakapokutana na sisi," ameongeza.
Kadhalika Amri Said amewaomba waamuzi watakaochezesha mechi hiyo kufuata sheria za soka bila kupendelea upande wowote ili mwenye uwezo na aliyejiandaa vizuri ashinde kihalali.
No comments:
Post a Comment