WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS KUHAMIA MKOANI DODOMA JANA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongaza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dodoma
katika mapokezi rasmi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan baada ya
kuhamia Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017. kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa salamu za kumkaribisha Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan aliyehamia rasmi Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Makamu
wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Januari
Makamba wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa
Rais Mkoani Dodoma leo Desemba 15, 2017.
Balozi Job Lusinde akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa Dodoma kwakuhamia Makamu wa Rais Mkoani Dodoma.
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.
Akizungumza
wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa
ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo
Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.
“Siku
ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza
Mhe. Samia
Aidha,
Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda ya kuifanya Dodoma
kuwa ya kijani hivyo wameandaa programu mbalimbali ikiwemo ya upandaji
miti .
“Tarehe
21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo
tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza
azma hii” ameongeza Mhe. Samia.
Kwa
upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Baba wa
Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia Dodoma tangu mwaka 1973 na leo
Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto hiyo.
“Tunaendelea
kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi
2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali
na kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine”
amefafanua Waziri Mkuu.
Naye
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras
Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya
Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.
“Sikuwaza
kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo
haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana
kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.
Kwa
upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais
anahamia Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo
imekuwa”.
Mbali
na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi
ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima,
hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha
kuandaa mashamba.
No comments:
Post a Comment